Darsa ya Ijumaa الزبيررضى الله عنه في غزوة بدر 🔴 LIVE Darsa (V)
Darsa ilifanyika Rabi'l Awwal 10, 1446 H Ijumaa Septemba 13, 2024
DARSA YA ARUBAINI NA TANO (45)
Kumi waliobashiriwa Jannah المبشرون بالجنة
"Amekujieni kuwafundisha Dini yenu.” " أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ "
Nani wanaoelekezewa maneno haya?! Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia)
عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ رضى الله عنه قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَبُو بَكْرٍ فِي الْجَنَّةِ وَعُمَرُ فِي الْجَنَّةِ وَعُثْمَانُ فِي الْجَنَّةِ وَعَلِيٌّ فِي الْجَنَّةِ وَطَلْحَةُ فِي الْجَنَّةِ وَالزُّبَيْرُ فِي الْجَنَّةِ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَوْفٍ فِي الْجَنَّةِ وَسَعْدٌ فِي الْجَنَّةِ وَسَعِيدٌ فِي الْجَنَّةِ وَأَبُو عُبَيْدَةَ بْنُ الْجَرَّاحِ فِي الْجَنَّةِ "
Kutokana na Abdur Rahman bin Awf (Allah Awe Radhi Nae) amesema kuwa: Rasuli wa Allah ﷺ amesema: "Abu Bakr katika Jannah, na Umar katika Jannah, na Ali katika Jannah, na Uthman katika Jannah, na Talha katika Jannah, na Az Zubair katika Jannah, na Abdur Rahmaan bin Awf katika Jannah, na Sa'd (bin Abi Waqqas) katika Jannah, na Said (bin Zaid katika Jannah, na Abu Ubaydah Ibn Jarrah katika Jannah."