top of page

 

 

YALIYOMO

 

Utangulizi wa Mfasiri        ……………………………………....     3

Utangulizi wa Mwandishi      .........................................................  12

Sehemu ya kwanza:

Ubainifu kuwa itikadi za maimamu wote wane ni moja katika mambo yote ya msingi ya Dini  .......................................................15

Sehemu ya pili:

Itikadi ya imamu Abu Hanifa  (Allah Amrehemu)

Kauli yake kuhusu Tawhidi   .......................................................... 21

Kauli yake katika kuzithibitisha Sifa za Allah na majibu yake dhidi ya Jahmiyyah  ................................ ................................................ 24

Kauli yake kuhusu Qadar     ......... ................................................. 33

Kauli yake kuhusu Imani   ...........................................................    39

Kauli yake kuhusu Swahaba (Allah Awe Radhi nao jamia) ..........  40

Msimamo wake dhidi ya ilmul-kalaam na malumbano katika Dini.42

Sehemu ya Tatu:

Itikadi ya imamu Malik bin Anas (Allah Amrehemu)

Kauli yake kuhusu Tawhidi  ..........................................................  46

Kauli yake kuhusu Qadar ............................................................... 53

Kauli yake kuhusu Imani ................................................................ 56

Kauli yake kuhusu Swahaba (Allah Awe Radhi nao jamia) ..........  58

Msimamo wake dhidi ya ilmul-kaalam na malumbano katika Dini.62 

Sehemu ya Nne:

Itikadi ya imamu Shafi  (Allah Amrehemu)

Kauli yake kuhusu Tawhidi  ........................................ ................. 66

Kauli yake kuhusu Qadar          ......................................................81

Kauli yake kuhusu Imani          .....................................................  85

Kauli yake kuhusu Swahaba (Allah Awe Radhi nao jamia) .......... 98

Msimamo wake dhidi ya ilmul-kaalam ........................................ 101

Sehemu ya Tano:

Itikadi ya imamu Ahmad bin Hanbal (Allah Amrehemu)

Kauli yake kuhusu Tawhidi          ................................................. 103

Kauli yake kuhusu Qadar         ... ..................................................107  

Kauli yake kuhusu Imani           .....................................................109    

Kauli yake kuhusu Swahaba (Allah Awe Radhi nao jamia) ..........112

Msimamo wake dhidi ya ilmul-kalaam  .......................................115

Hitimisho  .................................................................................... 118

Faharisi ya Vitabu   ..................................................................... 126

رب يسر ولا تعسر

 

Utangulizi wa Mfasiri

 

إنَّ الْحَمْدَ لِلهِ نَحْمَدُهُ وَنَسْتَعِينُهُ وَنَسْتَغْفِرُهُ، وَنَعُوذُ بِاللهِ مِنْ شُرُورِ أَنْفُسِنَا وَمِنْ سَيِّئَاتِ أَعْمَالِنَا، مَنْ يَهْدِهِ اللهُ فَلاَ مُضِلَّ لَهُ، وَمَنْ يُضْلِلْ فَلاَ هَادِىَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ.

Himda zote ni Zake Allah, tunamshukuru Yeye, na tunamtaka msaada, na tunamuomba Atuhidi, na tunatubia Kwake kwa dhambi na makosa yetu yote; na pia tunaomba hifadhi Kwake Allah kutokana na shari za (maovu ya) nafsi zetu, na ubaya wa amali zetu; yeyote yule ambae Allah Amemhidi, basi huwa hakuna wa kumpoteza, na yeyote yule aliyepotea, huwa hakuna wa kumhidi na wala hakuna uwezekano wa kumpatia msaidizi wa kumuongoza.

 

Nashuhudia kwamba hakuna Ilahi Apaswae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Mmoja Pekee, Ambae Hakuzaa wala Hakuzaliwa, na wala Hana mshirika yoyote yule; na ninashuhudia kuwa (Nabii) Muhammad ﷺ ni Mja Wake na ni Rasuli Wake wa mwisho; Rehema na Amani za Allah zimshukie yeye na wake zake na dhuria wake na jamaa zake, na Swahaba zake (Allah Awe Radhi Nao Jamia), na kila

anayewafuata kwa ihsani mpaka Siku ya Qiyamah[1]. Allah Anasema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾

 

“Enyi mlioamini! Muogopeni Allah vile Apasavyo kuogopwa; na wala msife isipokuwa na nyinyi ni Waislamu”[2], pia Allah Anasema:

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١

 

“Enyi watu! Mcheni Rabi wenu Ambae Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Adam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawa) na Akaeneza kutoka wawili hao wanaume wengi na wanawake (wengi pia); na mcheni Allah Ambae Kwake mnaombana na jamaa; hakika Allah Amekuwa juu yenu Raqiba (Mwenye kuchunga)”[3], pia Allah Anasema:

 

 

[1] Qiyamah (Kiyama): Siku ya kufufuliwa viumbe vyote na kusimama mbele ya Rabi wa walimwengu wote, Siku ambayo amali zao zitahudhurishwa na kuhesabiwa na kulipwa heri au shari; hii ni kusema kuwa hakuna siku wala hali yoyote ile katika masiku yetu na hali zetu za hapa duniani zenye kufanana au kuweza kuchukua wasifu wowote ule miongoni mwa wasifu wa Siku hii; hii ni Siku pekee ambayo tumetahadharishwa nayo, na kutakiwa tujiandae kwayo; na kubwa la hayo yote tunatakiwa tuiogope kwa yale yatakayotokea na kuwemo ndani yake; hivyo basi kwa Muumini ni vyema kutolitumia hili neno –Qiyamah/Kiyama- isipokuwa kwa matumizi yaliyotumiliwa na Dini yake.

[2] Aal Imraan 3:102.

[3] An Nisaa 4:1.

[1] Qiyamah (Kiyama): Siku ya kufufuliwa viumbe vyote na kusimama mbele ya Rabi wa walimwengu wote, Siku ambayo amali zao zitahudhurishwa na kuhesabiwa na kulipwa heri au shari; hii ni kusema kuwa hakuna siku wala hali yoyote ile katika masiku yetu na hali zetu za hapa duniani zenye kufanana au kuweza kuchukua wasifu wowote ule miongoni mwa wasifu wa Siku hii; hii ni Siku pekee ambayo tumetahadharishwa nayo, na kutakiwa tujiandae kwayo; na kubwa la hayo yote tunatakiwa tuiogope kwa yale yatakayotokea na kuwemo ndani yake; hivyo basi kwa Muumini ni vyema kutolitumia hili neno –Qiyamah/Kiyama- isipokuwa kwa matumizi yaliyotumiliwa na Dini yake.

[1] Aal Imraan 3:102.

[1] An Nisaa 4:1.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾ يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧١

“Enyi mlioamini! Mcheni Allah, na semeni kauli ya kweli (ya sawasawa); Atakutengenezeeni amali zenu, na Atakughufurieni dhambi zenu; na yeyote yule anayemtii Allah na Rasuli Wake ﷺ, basi amekwishafanikiwa mafanikio adhimu”[1].

 

أَمَّا بَعْدُ فَإِنَّ خَيْرَ الْحَدِيثِ كِتَابُ اللَّهِ وَخَيْرُ الْهُدَى هُدَى مُحَمَّدٍ وَشَرُّ الأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا وَكُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ ‏"‏ ‏.‏ 

 

Ama baada ya hayo! Kwa hakika, Hadithi iliyobora kabisa ni Kitabu cha Allah, na uongofu uliobora (na mzuri) kabisa ni uongofu wa Nabii Muhammad (ﷺ) na shari ya mambo (yote) ni yale mambo ya kuzushwa, na kila jambo la kuzushwa ni bidaa, na kila bidaa ni dhalala (upotevu)[2].

 

Namshukuru Allah kwa kuniwafikisha kuweza kukamilisha kazi hii ya kufasiri kitabu hichi, kazi ninayoamini kuwa ni miongoni mwa juhudi zinazolengwa kuhudumia Uislamu,

 

[1] Al Ahzaab 33: 70-71.

[2] Hii ni sehemu ya hutuba aliyokuwa akiitoa Rasuli wa Allah ﷺ kila anapohutubia kama ilivyothibiti katika Hadithi iliyopokelewa na maimamu wa Hadithi akiwemo Bukhari na Muslim; Bukhari katika Kitabu cha Kushikamana na Kitabu na Sunnah, mlango wa Kufuata Sunnah za Rasuli wa Allah ﷺ Hadithi namba (382); na Muslim, katika kitabu cha Ijumaa, mlango wa kuhafifisha Sala na Hutuba. Hadithi namba (1885). Hili ni lafdhi la Muslim. Kuna nyongeza isemayo: 'na kila dhalala –inapelekea kuingia- Motoni' ambayo iko kwa Nasaai, katika kitabu cha Sala za Idi mbili, mlango wa vipi kutolewa hutuba. Hadithi namba (1579).

kazi ambayo ninaamini kuwa itawanufaisha Waislamu wenzangu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili (hasahasa ahali wa darsa na mihadhara) kwa kuwafikishwa kuweza kuelewa karibu yale yote yenye kuhusiana na itikadi[1] ya Dini yao yenye ufafanuzi na maelezo wadhiha na wakutosheleza uliochotwa kutokana na kauli za Wanazuoni Rabbaniyyina[2]na ni Maimamu wenye kukubalika na kukubaliwa na Waumini kuwa ni watu wenye elimu sahihi na ufahamu uliosahihi kuhusu Allah, Rasuli Wake ﷺ na Dini Yake.

 

Kwa ujumla kazi hii inafungamana na itikadi anayotarajiwa kushikamana nayo kila Muislamu hususan wafuasi wa hawa maimamu; kazi hii ni juhudi moja ndogo kabisa miongoni

 

[1] Ni vyema ieleweke kuwa itikadi (aqida) ya Kiislamu ni Tawqifiyyah -kusudio lake ni kuwa: Kuthibiti kwake huwa kunategemea Wahyi pekee; yote kwa kuwa itikadi ni mambo lenye kufungamana na mambo ya ghaibu, na hakuna uwezekano wa kuweza kufikia kuelewa na kulifahamu jambo lolote lile miongoni mwa mambo ya ghaibu kwa kutumia akili au rai au ilmul kalaam (falsafa) na wala jitihada; ndio ikiwa manhaj ya Swahaba na kila mwenye kuwafikishwa kuwafuata kwa ihsani mpaka Siku ya Qiyamah katika sayansi ya itikadi imefungika na vyanzo viwili pekee; haitoki nje ya kilichokuja kwenye Kitabu cha Allah na Sunnah sahihi za Rasuli Wake ﷺ, ambapo viwili hivi vyote ni Wahyi.

[2] Allah Anasema:

 

وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾

“Bali: Kuweni wanazuoni Rabbaniyyiyna kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu.” Aal Imraan 3:79. Kusudio la wanazuoni Rabbaniyyiyna ni wale watekezaji kulingana na elimu yao waliyotunukia na Allah, au wanazuoni wenye kuwalea na kuwafundisha watu yale waliyoyasoma na kudurusu kutoka kwenye Kitabu ya kumpwekesha Allah katika kila chenye kumhusu Yeye (Subhaanah), au mwanazuoni mwenye kufundisha watu hatua kwa hatua; kwa kuanza cha kwanza na kidogokidogo mpaka kufikia kiwango cha juu.

[1] Ni vyema ieleweke kuwa itikadi (aqida) ya Kiislamu ni Tawqifiyyah -kusudio lake ni kuwa: Kuthibiti kwake huwa kunategemea Wahyi pekee; yote kwa kuwa itikadi ni mambo lenye kufungamana na mambo ya ghaibu, na hakuna uwezekano wa kuweza kufikia kuelewa na kulifahamu jambo lolote lile miongoni mwa mambo ya ghaibu kwa kutumia akili au rai au ilmul kalaam (falsafa) na wala jitihada; ndio ikiwa manhaj ya Swahaba na kila mwenye kuwafikishwa kuwafuata kwa ihsani mpaka Siku ya Qiyamah katika sayansi ya itikadi imefungika na vyanzo viwili pekee; haitoki nje ya kilichokuja kwenye Kitabu cha Allah na Sunnah sahihi za Rasuli Wake ﷺ, ambapo viwili hivi vyote ni Wahyi.

[1] Allah Anasema:

 

وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾

“Bali: Kuweni wanazuoni Rabbaniyyiyna kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu.” Aal Imraan 3:79. Kusudio la wanazuoni Rabbaniyyiyna ni wale watekezaji kulingana na elimu yao waliyotunukia na Allah, au wanazuoni wenye kuwalea na kuwafundisha watu yale waliyoyasoma na kudurusu kutoka kwenye Kitabu ya kumpwekesha Allah katika kila chenye kumhusu Yeye (Subhaanah), au mwanazuoni mwenye kufundisha watu hatua kwa hatua; kwa kuanza cha kwanza na kidogokidogo mpaka kufikia kiwango cha juu.

Kwa ujumla kazi hii inafungamana na itikadi anayotarajiwa kushikamana nayo kila Muislamu hususan wafuasi wa hawa maimamu; kazi hii ni juhudi moja ndogo kabisa miongoni mwa juhudi zinazojumuisha juhudi nyengine nyingi jabari ambazo hufanywa na wenye kujinasibisha na ahali wa Sunnah[1] kwenye nyanja mbalimbali, ikiwemo ya itikadi, na firaq (makundi), na tarjama, na sira, na tarehe, na tafsiri, au Hadithi na kadhalika.

 

[1] Ahali wa Sunnah na Jamaa (Ahlus Sunnah wal Jama’ah) ni: Istilahi inayotumiwa na wengi wetu pale tunapotaka kuthibitisha kuwa si katika ahali wa bidaa, bali ni miongoni mwa wenye kushikamana na Sunnah na Jamaa ya Waislamu. Hata hivyo, istilahi hii huwa inawalenga wale pekee wenye kufuata Sunnah –njia ya Rasuli wa Allah ﷺ kwa kushikamana na yale yote yaliyothibiti kutokana na Rasuli wa Allah ﷺ- na Jamaa’ah ni Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia), na kila anayewafuata kwa ihsani katika itikadi, kauli, muamala, akhlaq, amali, na mengineo mpaka Siku ya Qiyaamah. Kwa ufupi mtu kuweza kufikia kubaini kama yeye kweli ni miongoni mwa ahali wa Sunnah au ni katika ahali wa bidaa; kuna mambo matatu ambayo ni miongoni mwa mambo ya itikadi ambayo kuna mzozo, na mvutano, malumbano na mabishano baina ya Ahali wa Sunnah na wale wenye kwenda kinyume nao; hivyo basi mtu hutakiwa kuyachukuwa mambo hayo matatu kama ndio kipimo au alama yake ya kujipima itayomsaidia kuweza kujigundua ni miongoni mwa kundi lipi: la kwanza ni: Suala la Kuonekana Allah Akhera (Jannah); la pili ni: Suala la Kuzungumza kwa Allah, na tatu ni: Suala ya Allah kuwepo juu mbinguni na juu ya Arshi; kama alivyosema Sheikh Abdul Aziz Ar Rajhi (Allah Amhifadhi): 'Yule mwenye kuthibitisha kuwa Allah Ataonekana Akhera, na akathibitisha Maneno ya Allah, na kwamba Allah Anazungumza kwa herufi na sauti, na kwamba Maneno ya Allah yako kwa matamshi na maana na wala si mahuluku, na kwamba Allah Yuko juu Amelingana juu ya Arshi (kunakolingana na Utukufu Wake) Ametengana na viumbe Vyake, basi huyo ni miongoni mwa Ahali wa Sunnah na Jamaa, na yule mwenye kupinga mambo haya matatu, basi elewa kuwa huyo ni katika ahali wa bidaa.' Hidaayatur Rabbaaniyyah fiy Sharhil ´Aqiydati Twahaawiyyah 1:217.

firaq (makundi), na tarjama, na sira, na tarehe, na tafsiri, au Hadithi na kadhalika.

Kwa kweli kazi hii na nyengine nyingi mithili yake ni changamoto miongoni mwa changamoto zinazokabili umma kwa gharadhi ya kushajiisha wanaharakati na wenye kujinasibisha na ahali wa Sunnah hususan na wasomi wao kwa ujumla kutoa michango yao; iwe kwa kufasiri, au kuandika, au kudarasisha, au kuhadhiri na kadhalika; michango itayoweza kufikia kusahihisha, au kurekebisha, au kusawazisha pale panapoonekana kuwa panatakikana hayo katika jamii.
Kwa mintarafu hiyo basi, nimeona kuwa kuna haja na umuhimu wa kufasiri kitabu hichi –Itikadi ya Maimamu Wane اعْتهقَادُ الْئَهمَ ه ة الَْرْبَعَ ه ة - chenye kauli za hao maimamu, kauli zilizochotwa kutokana na ufahamu waliourithi na kushikamana na ufahamu wa Salaf9 wa Qur aani na Sunnah sahihi. 9 Salaf: Tamshi hili hutumika kwa kuzingatia mambo mawili: Jambo la kwanza kwa: Kuzingatia wakati (zama) Jambo la pili kwa: Kuzingatia kile chenye kuitakidiwa. Hivyo basi likitumiwa kwa kuzingatia zama huwa walengwa wake ni wale pekee waliokuwa katika karne tatu bora ambao Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم
ameshuhudia ubora wao, kama ilivyothibiti katika Hadithi:
عَنْ ه عمْرَانَ بْنَ حُصَيْنٍ  رضى الله عنهما  يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللََّّه صلى الله عليه وسلم " خَيْرُ
أُمَّتهي قَرْنهي ثُمَّ الَّ ه ذينَ يَلُونَهُمْ ثُمَّ الَّ ه ذينَ يَلُونَهُمْ ". قَالَ ه عمْرَانُ فَلاَ أَدْ ه ري أَذَكَرَ بَعْدَ
قَرْنه ه قَرْنَيْ ه ن أَوْ ثَلاَثًا " ثُمَّ إهنَّ بَعْدَكُمْ قَوْمًا يَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْ هَدُونَ، وَيَخُونُونَ
وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ، وَيَنْذُرُونَ وَلاَ يَفُونَ، وَيَظْهَرُ فهي ه همُ ال ه سمَنُ ".

Kutokana na Imrana bin Huswayni (Allah Awe Radhi Nao) anasema kuwa: Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلمamesema: “Waliobora wa umma wangu ni wale wa karne yangu -Swahaba Allah Awe Radhi Nao Jamia-, kisha wale ambao wanawafuatia –Taabiina –Rahimahumullahu Jamia-, kisha wale ambao wanawafuatia (Taabiina)." (Imrana Allah Awe Radhi Nae) akaongeza kwa kusema: ‘Sielewi –sikumbuki- kama Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم alitaja karne mbili au tatu baada ya karne yake ‘صلى الله عليه وسلم, kisha Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم akasema: “Kwa hakika baada yenu (watakuja) kaumu ambao watashuhudia bila ya kuombwa kufanya hivyo, na wanafanya khiyana na wala hawaaminiki, na wanaweka nadhiri (lakini) hawazitimizi, na utadhihirika kati yao unene." Wamewafikiana Bukhari na Muslim: Bukhari katika kitabu cha Fadhila za Swahaba wa Nabii صلى الله عليه وسلم , mlango wa Fadhila za Swahaba (Allah Awe Radhi nao) wa Nabii صلى الله عليه وسلم. Hadithi namba (2); na Muslim, katika kitabu cha Fadhila za Swahaba wa Nabii صلى الله عليه وسلم, mlango wa Fadhila za Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia), kisha wale ambao wanawafuatia, kisha wale ambao wanawafuatia. Hadithi namba (6156). Hili ni tamshi la Bukhari. Hii ni kusema kuwa kusudio la usemi huu Salaf: ni Swahaba na wale waliokuwa katika karne tatu bora. Ama likitumiwa kwa kuzingatia kile chenye kuitakidiwa wakati huo walengwa wake huwa kila anayeshikamana na kufuata manhaj ya Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia) na ya wale waliokuwa katika karne tatu bora katika itikadi na amali na mengineo mpaka Siku ya Mwisho. Angalia Hayaatus Salaf baynal Qawli wal ‘amali cha Ahmad bin Naaswir Twayyaar uk 8. Hivyo mtu anapodai kuwa anawafuata Salaf au anafuata manhaj ya (Salafiyyah) au yeye ni salafi hutakiwa aelewe kuwa kajinasibisha na Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia) na wale waliokuwa katika karne tatu bora, na kuwa anashikamana na yale yote waliyokuwa wameshikamana nayo hususan katika Dini na katika maisha kwa ujumla. Matumizi ya neno Salaf au Salafiyyah si mageni katika jamii ya Kiswahili; kwani Sheikh Farsi (Allah Amrehemu) katika maelezo yake ya Aayah ya 89 ya Suratul Baqarah alipokuwa akielezea kuhusu kutokubalika kuomba kwa jaha, alisema hivi: ‘Maneno haya hawakuyasema wale wafasiri wa mwanzo kabisa (Salaf) wenye kutegemewa, kama imamu Ibn Jarir..... Basi hiyo ya kuwa waliomba kwa jaha ya Mtume صلى الله عليه وسلم siyo NDIYO: ingawa imetajwa na wafasiri wengi wa nyuma baada ya hao Salaf wa kutegemea’. Ni wazi kabisa katika maelezo yake kuwa kinachotokana na Salaf ndio SAHIHI na ndio cha kukishikilia iwe kwenye itikadi, au tafsiri au manhaj na kadhalika; yote kwa kuwa –
10
Mwisho ni kuwa kazi yangu kubwa katika kitabu hichi ilikuwa kuweka au kupachika nyongeza zenye lengo la kufafanua, kuwadhihisha au kudalilisha pale nilipoona kuwa ni penye kuhitaji hilo, na kuziweka Hadithi kwa ukamilifu wake na kwa Takhrij10 zake na kila nilipofanya hilo husema: Mfasiri.
Ndugu yangu katika imani -Allah Akurehemu- tumia wakati wako adhimu upate kufaidika kusiko kadirika kwa kupata uhondo wa kuzisikia kauli za maimamu (Allah Awarehemu Jamia), kauli zenye kusisimuwa kwa mwenye kutaka kushikamana na kutafuta kufuata Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia) kwa ihsani jambo ambalo ni sharti katika kuweza kufikia kuridhiwa na Allah na kutunukiwa Jannah11; hivyo kama asemavo Sheikh Farsi (Rahimahullahu)- ni wa kutegemewa na wengine ni kinyume chake, kwa kuwa Salaf wameshikamana na Qur aani na Sunnah za Rasuli Wake صلى الله عليه وسلم kwa Muradi Wake Allah na kwa muradi wa Rasuli Wake صلى الله عليه وسلم.
10 Takhrij ni: Kuidhihirisha Hadithi kwa watu kwa kutaja wapokezi wake (yaani rijali wa mlolongo wake wa mapokezi ambao wameitowa Hadithi husika kutokana na tarika zao. Kwa mfano husema: Hadithi hii ameitowa Bukhari yaani: ameipokea na kutaja wapokezi wake. Au Kuifikisha Hadithi (na kile inachoashiria) kwenye vyanzo vyake vya asili vilivyonasibishwa (vitabu ambavo vimeisimulia kwa milolongo ya upokezaji kutoka kwa mwandishi hadi kufikia kwa Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم
kama vile Sahihi ya Bukhari na Muslim na kadhalika), na ikiwa hilo haliwezekani, basi kwa vyanzo vya pili vilivyonasibishwa, na kama hilo haliwezekani, basi kwa yule aliyeisambaza kwa milolongo yake ya upokezaji, aghlabu huwa pamoja na kubainisha daraja ya Hadithi husika (kama ni sahihi au dhaifu inapobidi). Angalia: Usulut Takhriji wa Diraasati Asaanid cha Dr. Mahmoud Twahhan, uk 9.
11 Allah Anasema:

basi nisikukoseshe uhondo, tafadhali wasikilize maimamu kwa makini kupitia masikio yako na macho yako, na kwa moyo mkunjufu; Allah Yu pamoja na Muhsinina.
Namuomba Allah Ajaaliye kazi hii iwe yenye ikhlasi yenye kutafuta Wajihi Wake; na Awalipe wale wote waliopelekea kukamilika kwa kazi hii (hususan wanadarsa katika mji wa Leicester, UK.) kila la heri duniani na huko Akhera. Allahuma Aamin.
Wakatabahu: Abu Fatmah Abdur Rauf A Abdul Kadir
Jumadal Ukh-ra 1438H - March 2017

وَالسَّابهقُونَ الْْوََّلُونَ ه منَ الْمُهَا ه ج ه رينَ وَالْْنَصَا ه ر وَالَّ ه ذينَ اتَّبَعُوهُم بهإهحْسَانٍ رَّ ه ض يَ
اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ ﴿ ١٠٠ ﴾
“Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhajirina na Ansari na wale waliowafuata kwa ihsani; Allah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye …....” At Tawbah 9:100.
12
Utangulizi wa Mwandishi
Hakuna shaka yoyote ile kwamba sifa njema zote zinamstahikia Allah Pekee; tunamhimidi (Yeye), na tunamtaka msaada, na tunamuomba Atuhidi na tunamuomba maghfira, na tunaomba hifadhi Kwake Allah kutokana na shari za nafsi zetu, na makosa ya amali zetu; yeyote yule ambaye Allah Amemuongoa, huwa hakuna wa kumpotosha, na yeyote yule anayepotea, basi huwa hakuna wa kumuongoa.
Nashuhudia kwamba hakuna Ilahi Anapaswaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Mmoja Pekee Asiye na mshirika; na ninashuhudia kwamba Muhammad صلى الله عليه وسلم ni Mja Wake na ni Rasuli Wake.
يَا أَيُّهَا الَّ ه ذينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاته ه وَلَا تَمُوتُنَّ إهلَّا وَأَنتُم
مُّسْ ه لمُونَ ﴿ ١٠٢ ﴾
“Enyi mlioamini! Muogopeni Allah vile apasavyo kuogopwa; na wala msife isipokuwa na nyinyi ni Waislamu”12, pia Allah Anasema:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّ ه ذي خَلَقَكُم ه من نَّفْسٍ وَا ه حدَةٍ وَخَلَقَ ه منْهَا
زَوْجَهَا وَبَثَّ ه منْهُمَا ه رجَالًا كَثهيرً ا وَنهسَاءً وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّ ه ذي تَسَاءَلُونَ
به ه وَالْْرَْحَامَ إهنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَ ه قيبًا ﴿ ١ ﴾
“Enyi watu! Mcheni Rabi wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Adam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawa) na Akaeneza kutoka wawili hao
12 Aal Imraan 3:102.
13
wanaume wengi na wanawake (wengi pia), na mcheni Allah Ambaye Kwake mnaombana na jamaa; hakika Allah Amekuwa juu yenu Raqiba (Mwenye kuchunga)”13; pia Allah Anasema: يَا أَيُّهَا الَّ ه ذينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَ ه ديدًا ﴿ ٧٠ ﴾ يُصْه لحْ لَكُمْ
أَعْمَالَكُمْ وَيَغْ ه فرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَمَن يُ ه طعه اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا
عَ ه ظيمًا ﴿ ٧١ ﴾
“Enyi mlioamini! Mcheni Allah; na semeni kauli ya kweli (ya sawasawa); Atakutengenezeeni amali zenu, na Atakughufurieni dhambi zenu; na yeyote yule anayemtii Allah na Rasuli Wake, basi amekwishafanikiwa mafanikio adhimu”14.
Ama baada ya hayo! Nimefanya utafiti wa kina katika masomo yangu ya uzamili, utafiti ulionipelekea kufikia kutunukiwa shahada ya PhD katika misingi ya Dini kulingana na imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu).
Basi katika utanguliza wa risala yangu niliambatanisha maelezo kwa muhtasari kuhusiana na itikadi ya maimamu watatu: Imamu Malik, imamu Shafi na imamu Ahmad bin Hanbal (Allah Awarehemu Jamia); basi kutokana na kuweko kwa maelezo hayo, baadhi ya watu wenye fadhila walinipendekezea kuandaa kijitabu kitakachoipwekesha itikadi ya maimamu watatu kwa lengo la kukamilisha kutaja itikadi ya maimamu wane.
Hivyo basi nimeonelea ni vyema kuambatanisha pamoja na yale niliyoyataja kwenye utangulizi wa utafiti wangu
13 An Nisaa 4:1.
14 Al Ahzaab 33: 70-71.
14
muhtasari wa yale niliyoyaeleza kwa kina kuhusiana na itikadi ya imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) katika Tawhidi, Qadar, Imani, Swahaba na msimamo wake dhidi ya ilmul kalaam (hoja za maneno matupu ya kiakili na falsafa).
Namuomba Allah Ajaaliye kazi hii iwe na ikhlasi kwa minajili ya kutafuta Wajihi Wake; na Atuwafikishe sote kwa pamoja kwenye uongofu wa Kitabu Chake na kushikamana na Sunnah za Rasuli Wake Muhammad صلى الله عليه وسلم; na Allah Yu nyuma ya kusudio, Naye Anatutosheleza, Naye ni Mbora wa kutegemewa. Na wito wetu wa mwisho ni kusema: Alhamdulillahi Rabbil ‘alamina.
Muhammad bin Abdur Rahmaan Al Khamis
15
Sehemu ya Kwanza Ubainifu kuwa itikadi ya maimamu wote wane (Allah Awarehemu Jamia) ni moja katika mambo yote ya msingi ya Dini isipokuwa katika suala la Imani
Itikadi ya maimamu wane ni itikadi ileile iliyotamkwa na Kitabu cha Allah na kuthibiti kwenye Sunnah sahihi za Nabii Muhammadصلى الله عليه وسلم, na ndio itikadi ileile waliyokuwa wameshikamana nayo Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia), na watu wa karne tatu bora na kila aliyewafikishwa kuwafuata kwa ihsani.
Hakuna mzozo wowote ule baina ya maimamu wane (Allah Awarehemu Jamia) katika misingi ya Dini, bali wao wote ni wenye kukubaliana juu ya imani kuhusiana na Sifa za Rabi, na kwamba Qur aani ni Maneno ya Allah na wala si mahuluku, na kwamba imani haina budi ndani yake kuwepo kusadikisha kwa moyo na kubaini kwa ulimi.
Maimamu wote wane (Allah Awarehemu Jamia) walikuwa wakiwapinga washabiki wa ilmul kalaam miongoni mwao Jahmiyyah15 na wengineo katika wale walioathirika na falsafa za Kiyunani na dhehebu la wanafalsafa.
15 Mfasiri: Ni pote lililoasisiwa na Ja’d ambae ndie aliyekuwa mtu wa kwanza anaeeleweka kuwa ndie aliyekuja na bidaa ya kuzungumzia kuhusiana na Sifa za Allah na kuzikanusha kwa kutumia akili yake. Ja’d alikuwa akikithirisha kwenda kwa Wahb bin Munabbih (miongoni mwa Tabiina wakubwa; Allah Amrehemu) na kuzijadili Sifa za Allah; Wahb (Allah Amrehemu) kwa Tawfiki ya Allah aliweza kufikia kugundua chanzo cha upotevu wake kwa kule kung’ang’ania kwake kujadili Sifa za Allah; Wahab alijaribu kumuwaidhi na kumuongoza kwenye manhaj sahihi, kwa kumuwekea bayana na wakati huohuo kumkataza na kumuonya na kumtahadharisha kwa kumwambia kuwa: Ole wako ewe Ja’d! Wacha kung’ang’ania kujadili masuala haya; hakika mimi nakuona
16
Shaikhul Islamu Ibn Taymiyyah (Allah Amrehemu) amesema: ‘Kutokana na Rehema za Allah kwa waja Wake kuwa walikuweko maimamu ambao wana lisani wenye kusema kweli katika umma; kama vile hawa maimamu wane (Allah Awarehemu Jamia) na wengineo ....., maimamu ambao walikuwa wakizipinga kauli za watu wa ilmul-kalaam miongoni mwao Jahmiyyah; walikuwa wakizipinga kauli zao zote za uzushi kuhusiana na Qur aani, na pia wakizipinga kauli zao kuhusu imani na kuhusu Sifa za Rabi. Na -hawa maimamu- walikuwa ni wenye kukubaliana juu ya yale waliyokuwa wameshikamana nayo Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia); kwamba Allah Ataonekana Akhera16, na
kuwa wewe ni miongoni mwa wenye kuhiliki; kwani lau Allah Hakutueleza katika Kitabu Chake kuwa:Ana Mkono, basi tusingelimthibitishia hilo, na kwamba: Ana Macho, basi tusingelimthibitishia hilo ....; na akataja sifa ya Elimu, na ya Kusema na nyenginezo. Miongoni mwa itikadi za pote hili ni kuwa: Qur aani ni mahuluku; na ukanushaji wa Sifa za Allah. Angalia Sharh Uswul I’tiqad Ahlus 1-2, uk.42-43.
16 Mfasiri: Kuna Hadithi nyingi sahihi zenye kuthibitisha kuwa Waumini watamuona Rabi wao Akhera; miongoni mwake ni hii: عَنْ أَبهي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه أَنَّ النَّاسَ، قَالُوا يَا رَسُولَ اللََّّه هَلْ نَرَى رَبَّنَا يَوْمَ
الْ ه قيَامَ ه ة فَقَالَ رَسُولُ اللََّّه صلى الله عليه وسلم " هَلْ تُضَارُّونَ فهي الْقَمَ ه ر لَيْلَةَ الْبَدْ ه ر ". قَالُوا لاَ يَا
رَسُولَ اللََّّ ه. قَالَ " فَهَ لْ تُضَارُّونَ فهي الشَّمْ ه س لَيْسَ دُونَهَا سَحَابٌ ". قَالُوا لاَ يَا
رَسُولَ اللََّّ ه. قَالَ " فَإه نَّكُمْ تَرَوْنَهُ كَذَ ه لكَ “…..
Kutokana na Abu Hurayrah (Allah Awe Radhi Nae) amesema kuwa: ‘Watu walisema: Ewe Rasuli wa Allah! Je, tutamuona Rabi wetu Siku ya Qiyaamah?’ Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم aliwajibu kwa kuwauliza: “Je, kwani mna tatizo lolote lile la kuuona mwezi usiku unapokuwa mpevu? Wakamjibu kwa kusema: ‘Hapana. Ewe Rasuli wa Allah!’ Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم
akawauliza tena kwa kusema: “Je, kwani mna shida yoyote ile ya kuliona jua na ilhali hakuna mawingu?” Wakamjibu kwa kusema: ‘Hapana. Ewe Rasuli wa Allah!’ Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم akasema: “Basi hakika nyinyi mtamuona (Rabi wenu) kama hivyo….” Wamewafikiana Bukhari na
17
kwamba Qur aani ni Maneno ya Allah na wala si mahuluku17, na kwamba imani bila shaka yoyote ile ni kusadikisha kwa moyo na kukiri kwa ulimi .....’18
Pia Shaikhul Islaam Ibn Taymiyyah amesema kuwa: ‘Kwa hakika maimamu wote mashuhuri (Allah Awarehemu) wanamthibitishia Allah Sifa Anazostahiki, na wanasema kwamba: Qur aani ni Maneno ya Allah na wala si mahuluku; na wanasema kuwa: Allah Ataonekana Akhera; hilo ndio dhehebu la Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia), na (ndio
Muslim: Bukhari katika kitabu cha Tawhidi, mlango wa Kauli ya Allah Ta’alaa: وُجُوهٌ يَوْمَئهذٍ نَّا ه ضرَة ﴿ ٢٢ ﴾ إهلَىٰ رَبه هَا نَا ه ظرَة ﴿ ٢٣ ﴾
“Nyuso siku hiyo zitanawiri. Zikimtazama Rabb wake.”Al Qiyamah 75:22-23. Hadithi namba (532); na Muslim katika kitabu cha Imani, mlango wa Kujuwa tariki ya Ru yah (Kumuona Allah). Hadithi namba (350) Hili ni lafdhi la Bukhari. 17 Mfasiri: Qur aani ni Maneno ya Allah kwa herufi zake na maana yake. Allah Ameitamka kwa namna Aliyotaka; na hiyo ni Sifa Yake ya Kusema miongoni mwa sifa za vitendo; hivyo basi si laiki kwa Muumini kuidadisi kwa hali yeyote ile. Imamu As-Sa’di (Allah Amrehemu) katika kufasiri Aayah hii: وَإهنْ أَحَدٌ ه منَ الْمُشْ ه ر ه كينَ اسْتَجَارَكَ فَأ هَ جرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّ ه ثُمَّ أَبْ ه لغْهُ
مَأْمَنَه ﴿ۚ ٦ ﴾
“Na ikiwa mmoja yeyote yule miongoni mwa washirikina atakuomba umlinde (hifadhi), basi mlinde mpaka asikie Kalamullah (Maneno ya Allah: Qur aan), kisha mfikishe mahali pake pa amani…. “; amesema kuwa: ‘Katika Aayah hii, kuna burhani ya wazi kuhusiana na mafundisho ya Ahali wa Sunnah wanaoitakidi kuwa Qur aani ni Maneno ya Allah na si mahuluku, kwa sababu Yeye Allah Ndiye Aliyeyasema (hayo maneno), na Akaihusisha Kwake Mwenyewe kuongezea sifa ya kielelezo chake; na hii inabatilisha dhehebu la Mu’tazila na wengineo wanaodai kuwa Qur aani ni mahuluku. Angalia Tafsiris Sa’adi.
18 Kitabulul Imani uk.350- 351, maelezo ya Muhammad Harras.
18
dhehebu la) wale wote waliowafuata kwa ihsani, kuanzia ahali wa baiti ya Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم na wengineo, na ndio dhehebu la maimamu wenye kufuatwa, kama Malik ibn Anas, na Thawri, na Layth ibn Sa’d, na Awza’i, na Abu Hanifa, na Shafi, na Ahmad (Allah Awarehemu Jamia).”19
Aliulizwa Shaikhul Islaam Ibn Taymiyyah kuhusiana na itikadi ya imamu Shafi (Allah Amrehemu), basi alijibu kwa kusema kuwa: ‘Itikadi ya imamu Shafi (Rahimahullahu) na itikadi ya Salaf wa umma huu kama Malik, na Thawri, na Awza’i, na Ibnul Mubarak, na Ahmad ibn Hanbal, na Ishaq ibn Rahawayh (Allah Awarehemu Jamia) ndio itikadi ileile ya wanazuoni wenye kufuatwa kama Fudhayl ibn Iyadh, na Abu Sulaiman Darani, na Sahl ibn Abdullah Tustari (Allah Awarehemu Jamia) na wengineo. Hapana mzozo wowote ule baina ya hawa maimamu na wale walio kama wao katika misingi ya Dini, na kadhalika Abu Hanifa (Rahimahullahu), kwani itikadi iliyothibiti kutokana na yeye katika Tawhidi20,
19 Minhajus Sunnah 2/106.
20 Mfasiri: Tawhidi ina vigawanyo vyake:
Cha kwanza ni: Tawhidir-Rububiyyah: Nayo ni kumpwekesha Allah katika Uumbaji, Uendeshaji wa mambo yote katika ulimwengu, Utoaji riziki, Mwenye uwezo wa kuhuisha na Kufisha, kwa kuamini kwamba Yeye Pekee Ndiye Aliyeumba kila kitu, Anayeruzuku na Kuendesha mambo yote, Hana mshirika, na kuamini kwamba Ufalme wote ni Wake Pekee.
Cha pili ni: Tawhidil-Uluhiyyah: Kuitakidi kuwa Allah Pekee Ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki. Maana yake ni kumpwekesha Allah katika ibada kwa kuelekeza ibada zote Kwake Pekee Subhaanahu bila ya kumshirikisha na yeyote yule au chochote kile.
Cha tatu ni: Tawhidil-Asmaa wasw-Swifat: Ni kumpwekesha Allah katika Majina Yake Mazuri, na Sifa Zake Tukufu, nako ni kuitakidi kuwa Allah Yuko na Majina Mazuri na Sifa Tukufu, Hafanani na yeyote katika Sifa Zake, na wala katika Majina Yake. Ni kumthibitishia Allah Sifa na Majina yote yaliyokuja kwenye Qur aani na Sunnah za Rasuli Wake صلى الله عليه وسلم, bila ya kuzigeuza Sifa hizo maana yake, au kuzipinga, au kuzifananisha au kizishabihisha na sifa za viumbe au kuzipa unamna. Yeye Amejipa Majina
19
na Qadar21 na mfano wa hayo ni yenye kuwafikiana na itikadi ya hawa; na itikadi ya hawa ndio itikadi ileile waliyokuwa wameshikamana nayo Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia) na wale waliowafuata kwa ihsani (Allah Awarehemu Jamia),
Mazurimazuri na Sifa Tukufu na Akawataka waja Wake wamuombe na kumtukuza kwa Majina na Sifa hizo.
21 Mfasiri: Qadar (Kadari/Makadirio) ni yale mambo yaliyokwishaandikwa (pitishwa), Aliyoyakadiria Allah kwa viumbe kulingana na Elimu Yake iliyosabiki na kulingana na Hekima Yake. Kuamini Qadar ni wajibu juu ya kila Muislamu, kwani ni nguzo moja miongoni mwa nguzo sita (6) za imani kama ilivyothibiti kwenye Hadithi sahihi yenye kueleweka kwa jila la Hadithi ya Jibril (Alayhis Salamu): عَ ه ن عُمَر بْن الْخَطَّا ه ب رضي اللهُ عنه قَالَ بَيْنَمَا نَحْنُ ه عنْدَ رَسُو ه ل اللََّّه صلى الله عليه وسلم ذَاتَ
يَوْمٍ إهذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَ ه ديدُ بَيَا ه ض الثه يَا ه ب شَ ه ديدُ سَوَا ه د الشَّعَ ه ر لاَ يُرَى عَلَيْ ه أَثَرُ
السَّفَ ه ر وَلاَ يَعْ ه رفُهُ ه منَّا أَحَدٌ حَ تَّى جَلَسَ إهلَى النَّبه يه صلى الله عليه وسلم فَأسَْنَدَ رُكْبَتَيْ ه إهلَى رُكْبَتَيْ ه
وَوَضَعَ كَفَّيْ ه عَلَى فَ ه خذَيْ ه وَقَالَ يَا مُحَ مَّد فَأخَْبهرْنهي عَ ه ن ا ه لإيمَا ه ن . قَالَ " أَنْ تُؤْ ه منَ
بهالِلَّه وَمَلاَئهكَته ه وَكُتُبه ه وَرُسُ ه ل ه وَالْيَوْ ه م الآ ه خ ه ر وَتُؤْ ه منَ بهالْقَدَ ه ر خَيْ ه ر ه وَشَ ه ر ه " .
Kutokana na Umar (Allah Awe Radhi Nae) amesema kuwa: Siku moja tulikuwa tumekaa na Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم, basi ghafla alitokea rajuli ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja miongoni mwetu aliyemtambua, alikwenda akakaa karibu na Mtume صلى الله عليه وسلم kwa kuweka magoti yake karibu na magoti yake (Mtume صلى الله عليه وسلم) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akauliza kwa kusema: ‘Ewe Muhammad! Nipashe habari kuhusu Imani’. Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم
alimjibu kwa kusema: “Ni kuamini Allah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake na Siku ya Mwisho, na kuamini Qadar kheri yake na shari yake.” Wamewafikiana Bukhari na Muslim: Bukhari katika kitabu cha Imani, mlango wa Swali la Jibril (Alayhis Salamu) kwa Nabii صلى الله عليه وسلم kuhusu Imani, na Uislamu, na Ihsani, na Ujuzi (wa Kujuwa lini kitakuwa) Qiyamah. Hadithi namba (48); na Muslim katika kitabu cha Imani, mlango wa Ubainifu wa Imani, na Uislamu, na Ihsani, na Kwamba Imani Inalazimu Kuthibitisha Qadar, na Kubainisha dalili za kujiweka mbali na kuwakataa wale wasioamini Qadar, na kuwa na kauli kali dhidi yao. Hadithi namba (1) Hili ni lafdhi la Muslim.
20
na ndio itikadi ileile iliyotamkwa na Kitabu cha Allah na kuthibiti kwenye Sunnah za Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم’22.
Na haya ndiyo yale aliyoyahitari mwanachuoni Sadiq Hassan Khan (Allah Amrehemu) pale aliposema: ‘Dhehebu letu ndio dhehebu lile la Salaf, (ambalo ni) kuthibitisha (ithbaat: uthibitisho usiokuwa na ufananisho) bila ya tashbihi, na kuepusha (tanzih), na bila ya kukanusha, na kukataa (ta’twiyl); na ndio dhehebu la maimamu wa Kiislamu kama Malik, na Shafi, na Thawri, na Ibnul Mubarak, na Ahmad na wengineo (Allah Awarehemu Jamia); kwa uhakika hakuna mzozo wowote ule baina ya hawa maimamu katika misingi ya Dini; na kadhalika Abu Hanifa (Allah Amrehemu), kwani hakika itikadi iliyopokelewa kutokana nae ni itikadi ileile yenye kuwafikiana na itikadi ya hawa, na ndiyo ambayo imetamkwa na Kitabu cha Allah na Sunnah za Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم’23.
Hapa pana baadhi ya kauli za hawa maimamu wane: Abu Hanifa, Malik, Shafi na Ahmad (Allah Awarehemu Jamia) katika yale wanayoyaitakidi katika mambo ya msingi ya Dini pamoja na ubainifu wa misimamo yao dhidi ya ilmul-kalaam24.
22 Majmuu’u Fatawa 5/256.
23 Qatwfuth Thamar uk. 47-48 .
24 Mfasiri: Ilmul-kalaamu [Elimu ya akili na hoja; falsafa] kama inavyodaiwa ni: Elimu ya elimu zote, elimu ya asili ya mambo yote na vitu vyote, elimu ya kuelewa sababu na maana; taz. A standard English-Swahili Dictionary; pia taz. Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Washabiki wake wanasema kuwa falsafa ni: Kutumia akili katika kuutafuta ukweli.

Sehemu ya Pili
Itikadi ya imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) Kauli za imamu Abu Hanifa kuhusu Tawhidi. Kwanza: Itikadi ya imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) kuhusiana na Tawhidullahi25 na ubainifu wa hukumu ya tawasali26 za kisharia na ubatilifu wa tawasali zilizozushwa.
25 Mfasiri: Ni vyema hapa kuelezea kuwa hizi istilahi tulizonazo katika zama hizi zenye gharadhi ya kuwadhihisha aina (vigawanyo) vya Tawhidi: Tawhidul-Uluhiyyah, Tawhidur-Rububiyyah, na Tawhidul-As-maa wasw Swifat; istilahi hizi hazikuwekwa na Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم, na wala Swahaba zake (Allah Awe Radhi Nao Jamia); yote kwa kuwa katika zama zao, hakukuwepo haja ya kuigawanya Tawhidi katika vigawanyo vyenye lengo la upambanuzi na uchambuzi, ndio ikawa ni jambo la nadra kukutana na matumizi ya istilahi kama hizi katika matamshi na maandishi yao; bali tunachoweza kukutana au kukiona ni yale maelezo yao yenye kuhusiana na Tawhidullah yenye kumaanisha kwa ujumla kuwa Tawhidi ni mada moja yenye kushikamana kutokana na ufahamu wa watu wa zama zao; hivyo ndivyo walivyokuwa wakimaanisha kila wanapotaja neno au istilahi Tawhidullah; kwa kuwa ni istilahi yenye kujumuisha vipengele vyote vya Tawhidi vyenye kumaanisha kumpwekesha Allah kwa yale yote yanayomuhusu Allah. Vigawanyo vya Tawhidi vilitumiwa na wanazuoni waliokuja nyuma kutokana na kuweko haja ya kuigawanya, kuichambua na kuiwadhihisha Tawhidi katika zama zao, kutokana na ufahamu wa watu wa zama zao, ufahamu uliochanganyika na mafundisho ya dini walizokutana nazo, na falsafa iliyozagaa na kushamiri katika jamii zao. Wanazuoni wa nyakati hizo (Allah Awarehemu Jamia) baada ya kuiona hatari itayowasibu na inayowakabili Waislamu walihisi kuwepo umuhimu wa kuweka hivi vigawanyo vya Tawhidi kwa lengo la uchambuzi na ufafanuzi; hata hivyo, misingi yote ya vipengele vya vigawanyo hivi kwa uwazi kabisa inapatikana kwenye Qur aani na Sunnah sahihi za Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم.
26 Mfasiri: Kuna maneno mawili yenye kutumiwa kwa kumaanisha jambo moja; kwa kuwa maana zao zinakaribiana, neno la kwanza ni: Wasila (pia huandikwa Wasila au Wasilah; neno hili halipatikani kwenye Kamusi ya
22
1. Kuhusiana na Tawhidullahi imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: Haijuzu kwa mmoja yeyote yule kumuomba Allah isipokuwa kwa kupitia Kwake27, na (kumuomba kwa kutumia) dua zilizoidhinishwa kama vile inavyofaidika kutokana na Kauli Yake Ta’alaa:
وَ ه للَّ ه الْْسَْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ ه بهَا وَذَرُوا الَّ ه ذينَ يُلْ ه حدُونَ فهي أَسْمَائه ه
Kiswahili Sanifu): Katika lugha ya Kiarabu neno hili lina maana kuwa: Njia au sababu inayoweza kukufikisha utakapo; Allah Anasema:
يَا أَيُّهَا الَّ ه ذينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إهلَيْ ه الْوَ ه سيلَةَ وَجَا ه هدُوا فهي سَبهي ه ل ه لَعَلَّكُمْ
تُفْ ه لحُونَ﴿ ٣٥ ﴾
“Enyi mlioamini! Mcheni Allah na tafuteni Kwake Wasilah (njia za kumkurubia).” Al Maidah 5:35. Sheikh Al Farsi (Allah Amrehemu) katika kulieleza neno hili (Wasila) amesema: Ni jambo linalomfikisha mtu mahala fulani au linalomfikishia (linalompatia) kitu fulani; angalia maelezo yake kwenye Tafsiri ya Aayah ya 35 ya Suratul Maaidah. Neno la pili ni Tawasali (Tawasul) ambalo ni: Kumuomba Mungu kwa kuyaunganisha maombi hayo na baraka au jaha ya mtu au watu wenye cheo kwa Mungu. Angalia Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Maana hii iliyowekwa kwenye Kamusi inapingana na kupinzani kulikowazi kabisa na mafundisho sahihi ya Kiislamu; yote kwa kuwa katika Uislamu anaetakiwa kuombwa ni Allah Pekee bila ya kupitia kwa yeyote yule na bila ya kuunganisha maombi hayo na baraka au jaha, au cheo cha mtu au watu; kwani kumuomba Allah kwa kuunganisha maombi iwe kwa haki ya Nabii Muhammad صلى الله عليه وسلم au jaha (heshima) yake au ya yeyote yule miongoni mwa Mitume صلى الله عليه وسلم au watu wema au baraka au dhati ni katika uzushi, bali ni katika njia zenye kumpelekea muombaji kutumbukia kwenye ushirikina. Na jambo hili la kumuomba Allah kwa kuyaunganisha maombi hayo na baraka au jaha ya mtu au watu wenye cheo kwa Allah kama lingelikuwa ni katika amali njema na yenye kukubalika au yenye kufaa kufanywa, basi wangelitusabiki kwa hilo Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia) ambao ni wenye kumuelewa na kumjua zaidi Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم na haki yake na jaha yake صلى الله عليه وسلم; taz. Tawasulil Mashru’ wat Tawasulil Mamnu’ cha Sheikh Abdul Aziz bin Baaz na Sheikh Muhammad bin Swalih Uthaymiyn (Allah Awarehemu).
27 Durul Mukhtar pamoja na Hashiyatu Radul Mukhtar (6/396-397).
23
“Na Allah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo; na waacheni wale wanaopotosha (kwa kuharibu utukufu, kukanusha, kugeuza maana) katika Majina Yake ………….”28
2. Ama kuhusiana na tawasali imamu Abu Hanifa amesema: ‘Inachukiza kwa muombaji (dua) yeyote yule (kuomba) kwa kusema: Nakuomba kwa haki ya fulani au kwa haki ya Manabii Wako na Rasuli Zako صلى الله عليه وسلم au kwa haki ya Baitil Haraam (Baiti Tukufu) na Mash’aril Haraam’ 29.
3. Pia Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Haitakikani kwa mmoja yeyote yule kumuomba Allah isipokuwa kwa kupitia Kwake, na (anasema) nachukia (kwa muombaji dua yeyote yule kuomba) kwa kusema: (Nakuomba) kwa hadhi ya utukufu wa matendegu ya Arshi Yako30 au kwa haki ya viumbe Vyako’31.
28 Al A’araaf 7:180.
29 Sharhul Aqidatutw Twahawiyyah, uk.234, na It-hafus Sadatil Muttaqina 2/285, na Sharhul Fiqhil Akbar cha Qaariy uk 198.
30 Imamu Abu Hanifa na Mohammad ibnil Hassan walichukia mtu kusema katika dua zake: ’Ewe Rabi! Hakika mimi nakuomba kwa utukufu wa matendegu ya Arshi Yako’ kwa kutokuweko andiko lenye kuruhusu hilo, ama Abu Yusuf (Allah Amrehemu) alijuzisha hilo kutokana na kuwepo kwa mapokezi; ambayo ndani yake imesimuliwa kwamba Nabii صلى الله عليه وسلم
ilikuwa miongoni mwa dua zake akisema:
اللهم إني أسألك بمعاقد العز من عرشك ومنتهى الرحمة من كتابك
“Ewe Rabi! Hakika mimi nakuomba kwa utukufu wa matendegu ya Arshi Yako, na kwa ukubwa wa Rehema Yako kutokana na Kitabu Chako”. Hadithi hii ameitoa Bayhaqi katika Kitabu cha Da’watil Kabirah kama ilivyo kwenye Binayah (9/382) na Naswbur Rayah (4/272), katika isnaad (silsila ya mapokezi) yake kuna ila tatu:
1. Kutosikia Dawud bin Abi Aswim kutoka kwa Ibn Mas’ud (Allah Awe Radhi nae).
24
Pili:
Kauli yake katika kuthibitisha Sifa za Allah
na majibu yake dhidi ya Jahmiyyah.
4. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Allah Hasifiwi kwa sifa za viumbe; hivyo basi Ghadhabu Zake, na Ridhaa Yake ni sifa mbili miongoni mwa Sifa Zake bila kusema: Zikoje? Na hiyo ndio kauli ya Ahali wa Sunnah. Na Yeye Anaghadhibika na Anaridhia; na wala haisemwi kwamba: Ghadhabu Zake ni Ikabu Yake, na Ridhaa Yake ni Thawabu Zake. Na tunamsifu (Allah) namna vile Alivyojisifia Nafsi Yake Mwenyewe: kwamba ni Ahadun (Mmoja Pekee) Swamadu (Mwenye kukusudiwa kwa haja zote) Hakuzaa na wala Hakuzaliwa na wala haiwi Awe na yeyote anaefanana (au kulingana) Naye; Hayyun (Aliyehai daima) Qadirun (Muweza) Sami’un (Mwenye kusikia yote) Baswirun (Mwenye kuona yote) Alimun (Mjuzi wa yote); Mkono wa Allah Uko juu ya mikono yao; Mkono Wake si kama mikono ya viumbe Vyake, na Wajihi Wake si kama wajihi za viumbe Vyake’32.
2. Abdul Malik bin Jurayj ni mudallis (mwenye kuileta Hadithi kwa silsila yenye kudhanisha kwamba iko juu kuliko ilivyo uhakika wake kwa kushindwa kuonyesha imepokelewa kutoka wapi), na ni mwenye kuipandisha Hadithi moja kwa moja kwa Mtume صلى الله عليه وسلم bila ya kuonyesha imetokana na Swahaba gani.
3. Umar bin Harun anatuhumiwa kuwa ni muongo; na kwa minajili hiyo basi amesema Ibnul Jawziy kama kwenye Binayah (9/382): Hii ni Hadithi Mawdhuu’ (iliyozuliwa na kutungwa) bila ya shaka yoyote ile, na mlolongo wa wapokezi wake umeanguka hauna faida kama unavyouona. Taz. Tahdhibut Tahdhib (3/189), (6/405) na (7/501); na Taqribut Tahdhibu (1/520).
31Tawassul wal Wasilah, uk.82; pia taz: Ufafanuzi wa Fiqhul Akbar, uk. 198.
32 Fiqhul Absatw, uk.56.
25
5. Na akasema kuwa33: ‘Allah Ana Mkono, na Uso na Nafsi, kama Alivyovitaja Allah ndani ya Qur aani; basi vile Alivyovitaja Allah kwenye Qur aani katika kutaja Uso, na Mkono na Nafsi, hizo ni Sifa Zake bila ya zikoje; na wala haisemwi kuwa Mkono Wake ni Uwezo Wake au ni Neema Zake, kwa kuwa kusema hivyo ni kubatilisha Sifa na hiyo ni kauli ya ahali wa Qadar34 na ahali wa ‘Itizaal’35.
33 Fiqhul Akbar uk.302
34 Mfasiri: Ahali wa Qadar (Qadariyyah): Ni jina lililotumiwa na Ahali wa Sunnah kwa wale wote wenye kudai kuwa wao wenyewe (nafsi zao) ndio wenye kuumba matendo yao pasina Allah. Qadariyyah ni kundi la kwanza kuchomoza katika umma na ilikuwa wakati wa mwisho wa kipindi cha Swahaba (Allah Awe Radhi nao jamia), kundi hili linaongozwa na Ma’badul Juhaniy kwa kuwa yeye ndie mtu wa kwanza aliyekuja na bidaa ya kukanusha Qadar mjini Basra, kwa kusema kuwa mambo ni sawasawa -yako bure tu- kwamba haikusabiki Qadar wala Elimu kutoka kwa Allah, na kwamba Allah Anayajua baada ya kutokea kwake. Kundi hili linakana Qadar (nguzo ya sita katika nguzo za imani) na kusudio la kauli yao ni kuwa: Viumbe wenyewe ndio wenye kuumba matendo yao na kwamba Allah Hayajui hayo matendo ila baada ya kutokea kwake; au husema kuwa: Chochote kinachotokea hakitokani na Qadar, na wala Qadhaa ya Allah, bali ni jambo linalotokana na matendo ya mja mwenyewe, bila ya hukumu ya kabla kutoka kwa Allah. Angalia, Mawsu’al-Muyassarah fil Adyan wal-Madhahib wal-Ahzabil-Mu’aswirah. 35 Mafasiri: Ahali wa ‘Itizaal (Mu’tazila) ni: kila mwenye kukadimisha akili mbele ya Nusi; kundi hili hunasibishwa na Wasil bin Ataa kwa kuwa yeye ndie muasisi wake, kundi hili hubainika kwa kule kung’ang’ania kwao kutanguliza akili mbele ya Nususi. Huyu Wasil aliwahi kuwa mwanafunzi wa Hasanil Basri (Allah Amrehemu), na ndie mtu wa kwanza aliyeanzisha bidaa ya kuwa fasiki huwa yuko baina ya manzila mbili –kusudio lao ni kuwa fasiki kwa kule kutenda dhambi kubwa huwa si Muislamu, na wakati huohuo huwa si kafiri, bali huwa yuko baina wa wawili hao- hapa duniani. Wasil aliona kuwa mtenda dhambi kubwa (fasiki) hawezi kumtoa kwenye Uislamu (hawezi kumkufurisha kama wafanyavo wenye kuwakufurisha Waislamu kwa kule kushikamana na bidaa iliyozushwa na Khawarij) na wakati huohuo hawezi kumkufurisha kwa kumtumbukiza kwenye shimo la ukafiri; hivyo basi akawa hana pa kumuweka, ndipo
26
6. Na amesema kuwa: ‘Haitakikani kwa mmoja yeyote yule kusema kitu chochote kile kuhusiana na Dhati ya Allah, bali anatakiwa amsifu (Allah) kwa yale Aliyojisifia kwayo Nafsi Yake; na wala asisema ndani yake kitu chochote kile kwa (kutumia) rai (akili) yake, Amebarikika Allah Rabi wa walimwengu’36.
7. Na pale alipoulizwa kuhusiana na Ushukaji wa Kiungu. Alijibu kwa kusema: ‘(Allah) Hushuka bila ya kaifa (vipi)’37.
8. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema38: ‘Allah Huombwa kwa juu na wala sio kwa chini, hii ni kwa kuwa chini sio kitu chochote kile katika Sifa za Rububiyyah na wala Uluhiyyah’.
alipokuja na hii bidaa yake: kuwa fasiki huwa yuko baina ya manzila mbili. Basi pale Wasil alipodhihirisha bidaa yake hii (yenye kuhusiana na hukumu ya mtenda dhambi kubwa) katika majilisi ya Hasanul Basri (Rahimahullahu) ndio pakazuka hilafu baina yake na mwalimu wake ambae kwa upande wake baada ya kumbainishia kwa hoja na burhani bayana kuwa alichokisema sio sahihi, bali ni jambo la bidaa katika Dini, kwa kuwa halina dalili wala ushahidi wowote ule si kutoka kwenye Kitabu cha Allah na wala Sunnah za Rasuli Wake صلى الله عليه وسلم, na wala si katika kauli za Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia), Wasil aliamua kushikilia kile akitakacho baada ya ubainifu wote huo, hapo ndio Hasanul Basri (Allah Amrehemu) alipoamua kumfukuza kwenye majilisi yake, na kumpelekea kujitenga na kujichukulia uamuzi wa kuanzisha majilisi yake ili apate fursa ya kueneza bidaa yake; jambo lililopelekea kupewa hili jina la Mu’tazila na kila aliyemfuata. Na katika bidaa walizozusha ni kama hizi: Kukanushia Sifa za Allah za Azali; kukanusha kuonekana kwa Allah kwa macho huko Akhera. Angalia, Mawsu’al-Muyassarah fil Adyan wal-Madhahib.
36Sharhul Aqidatutw Twahawiyyah, 2/427 iliyohakikiwa na Dr Turki, Jala’ul’Aynan, uk. 368.
37 Aqidatus Salaf Aswhabil Hadithi, uk.42, na Asmaa wasw Swifat cha Bayhaqi, uk. 456, na Kawthari hakusema chochote kuhusiana na hili, na Sharhul Aqidatutw Twahawiyyah, uk. 245, iliyohakikiwa na imamu Albani, na Sharhul Fiqhil Akbar, ya Qaariy uk.60.
38 Fiqhul Absatw, uk.51.
27
9. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Naye (Allah) Anaghadhibika na Anaridhia na wala haisemwi kuwa Ghadhabu Zake ni Ikabu Yake na Ridhaa Yake ni Thawabu Zake39’.
10. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na wala Hashabihiani na kitu chochote kile katika vitu miongoni mwa viumbe Vyake; na wala Hashabihiani na kiumbe chochote kile katika viumbe Vyake40; daima abadi (Allah) Amekuwa na Ataendelea kusifika kwa Majina Yake Mazuri na Sifa Zake Tukufu’41.
11. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na Sifa Zake (Allah) ni tofauti kabisa na sifa za viumbe; Anajua sio kama tujuavo sisi; Anaweza sio kama tuwezavo sisi, Anaona sio kama tuonavo sisi, Anasikia sio kama tusikiavo sisi, Anasema sio kama tusemavo sisi’42.
39 Fiqhul Absatw, uk.56.
40Mfasiri: Kuhusiana na tashbihi (kushabihisha): Haafidh Nu’ayman bin Hammad amesema: ‘Yeyote yule mwenye kudai kuwa Allah Anashabihiana na viumbe Vyake basi huyo huwa amekufuru, na yeyote yule mwenye kukanusha kile ambacho Allah Amejisifia Nafsi Yake Mwenyewe kwacho pia huwa amekufuru. Na ni vyema ieleweke kuwa hakuna tashbihi kwa hali yoyote ile katika yale yote ambayo Allah Amejisifia kwayo Nafsi Yake Mwenyewe, au yale yote ambayo Rasuli Wake صلى الله عليه وسلم amemsifia kwayo’. Taz. ‘Uluww (uk. 217). Imamu Ishaaq bin Raahawayh amesema kuwa: ‘Tashbihi itapatinaka pale mtu atapodai kuwa: Mkono wa Allah ni kama mkono wangu au Usikivu wa Allah ni kama usikivu wangu na kadhalika; hii ndio tashbihi; lakini pale mtu anaposema: Mkono, Kuona na Kusikia kwa Allah ni kama Alivyosema Allah Mwenyewe katika Qur aani, kisha hatakiwi kuuliza vipi, na wala namna gani; huku hakuwezi kuwa tashbihi’. Mukhtaswarul ‘Uluww (uk. 191).
41 Fiqhul Akbar, uk.301.
42 Fiqhul Akbar, uk. 302.
28
12. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Allah Hasifiwi kwa sifa za viumbe’43.
13. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na yeyote yule atakayemsifu Allah kwa (kutumia) maana miongoni mwa maana (zinazotumiwa na) watu basi atakuwa amekufuru’44.
14. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na Sifa Zake ni za namna mbili: Sifa za kidhati na Sifa za kivitendo, ama zile za kidhati ni: Uhai, na Uwezo, na Ujuzi (Elimu), na Kusema, na Kusikia, na Kuona na Kutaka (Irada). Ama zile za kivitendo ni: Uumbaji, Utoaji wa riziki, Uanzilishaji, na Utengenezaji na zisizokuwa hizo miongoni mwa sifa za kivitendo; Allah Hatosita na Ataendelea kwa Majina Yake na kwa Sifa Zake’45.
15. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na Allah tokea azali Hakusita kuwa Mwenye kutenda kwa Utendaji Wake, na utendaji ni sifa katika azali, na Mtenda ni Yeye Subhaanah; na mtendwa ni mahuluku, na Utendaji wa Allah sio mahuluku’46.
16. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Yeyote yule atayesema kuwa: Sielewi kama Rabi wangu Yuko juu mbinguni au ardhini, atakuwa ameshakufuru; kadhalika (ameshakufuru) yeyote yule atayesema kuwa: Yeye (Rabi) Yu
43 Fiqhul Akbar, uk.56.
44 Aqidatutw Twahawiyyah, uk.25, iliyohakikiwa na Albani.
45 Fiqhul Akbar, uk.301.
46 Fiqhul Akbar, uk.301.
29
juu ya Arshi47, lakini sielewi kama hiyo Arshi iko mbinguni au ardhini’48.
17. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kumjibu mwanamke aliyemuuliza: ‘Yuko wapi Rabi wako unayemuabudu?’ Imamu Abu Hanifa akamjibu kwa kusema: ‘Hakika Allah (Ambae Ndie Rabi wangu ninayemuabudu) Yu juu mbinguni pasina ardhini’. Basi mtu akamwambia: Je, unasemaje kuhusiana na Kauli ya Allah:
وَهُوَ مَعَكُمْ ﴿ ٤ ﴾
“Naye (Allah) Yu Pamoja nanyi (kwa Ujuzi Wake) ....”49 Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) akajibu kwa kusema: ‘Hiyo ni kama unavyomuandikia mtu: Kuwa hakika mimi niko pamoja nawe na ilhali wewe uko ughaibuni.’50
18. Na akasema hivyohivyo: ‘Mkono wa Allah Uko juu ya mikono yao, Mkono Wake si kama mikono ya viumbe Vyake’51.
47Mfasiri: Shaikhul Islamu Ibn Taymiyyah (Allah Amrehemu) amesema kuwa: Mtu wa kwanza katika Uislamu aliyekuja na uzushi wa kusema kuwa Allah Hayuko juu ya Arshi kwa uhakika na kwamba maana ya Istiwaa (kulingana kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Sub-haanah) ni istawlaa (kutawala) na mfano wa haya ya bidaa ni Ja’d bin Dirham, na aliichukuwa bidaa hii kutoka kwa Jahm bin Swafwan na kuidhihirisha, na ndio ikanasibishwa hii kauli kwake.
48Fiqhul Absatw, uk. 46, na tamshi kama hili limenukuliwa na Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah katika Majmuu’ Fatawa (5/48), na Ibnul Qayyim katika Ijitima’ul Juyushil Islamiyyah, uk. 139, na Dhahabi katika ‘Uluww, uk. 101-102, na Ibnu Qudamah katika ‘Uluww, uk.116, na Ibn Abi ‘Izzi katika Sharhut Twahawiyyah uk. 301.
49 Al Hadiyd 57:4.
50 Asmaa wasw Swifat, uk.429.
51 Fiqhul Absatw, uk.56.
30
19. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Hakika Allah Yu juu mbinguni pasina ardhini’. Basi mtu akamwambia: Je, unasemaje kuhusiana na Kauli ya Allah:
وَهُوَ مَعَكُمْ ﴿ ٤ ﴾
“Naye (Allah) Yu Pamoja nanyi (kwa Ujuzi Wake)”52. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) akajibu kwa kusema: ‘Hiyo ni kama unavyomuandikia mtu: Kuwa hakika mimi niko pamoja nawe na ilhali wewe uko ughaibuni’53.
20. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘(Allah) Alikwishakuwa Mwenye kusema54 (tokea azali) na wala Hakuwa hivyo (Mwenye kusema) kwa kumsemesha Musa صلى الله عليه وسلم’ 55.
52 Al Hadiyd 57:4.
53 Asmaa wasw Swifat, 2/170.
54 Mfasiri: Imamu Suyutwi (Allah Amrehemu) amesema (katika kitabu cha Al Awaail): kuwa: Mtu wa kwanza miongoni mwa wale waliotamka neno habithi katika itikadi –katika Uislamu- alikuwa ni Ja’d bin Dirham .... Ja’d alikuja na bidaa ya kudai kuwa: Allah Hasemi. Ja’d alidhania –kwa kule kukadimisha akili yake mbele na Nususi- kuwa ataweza kufikia kumpwekesha Allah vile Anavyostahiki kupwekeshwa, jambo lililomshinikiza na kumsukuma kufikia kukanusha Sifa za Allah alizodhania kuwa akizithibitisha atakuwa anammithilisha Allah na viumbe Vyake; na miongoni mwa sifa hizo ni hii sifa ya Kusema, basi kule kuikanusha kwake sifa hii ndio kulikomshinikiza kuja na bidaa ya kusema kwamba: Qur aani ni mahuluku, na akakanusha kwamba Allah Ametamka Qur aani kwa uhakika na pia akakanusha kwamba Allah Amemchukua Ibrahim صلى الله عليه وسلم kuwa ni khalili. Jahm aliichukuwa bidaa hii na njengine nyingi na kuzidhihirisha, na ndio ikaegemezwa kwake. Hivyo basi Jahm siye mtu wa kwanza aliyekuja na bidaa ya kudai kuwa Qur aani ni mahuluku, bali aliichukuwa bidaa hiyo kutokana na Ja’d bin Dirham.
55 Fiqhul Akbar, uk.302.

21. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘(Allah) ni Mwenye kusema kwa Maneno Yake na Maneno ni sifa tokea azali’ 56.
22. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘(Allah) Anasema (na huko kusema Kwake) sio kama tusemavo sisi’57.
23. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na Musa صلى الله عليه وسلم alisikia Maneno ya Allah, kama Alivyosema Allah katika Qur aani:
وَكَلَّمَ اللَّهُ مُوسَىٰ تَكْ ه ليمًا ﴿ ١٦٤ ﴾
“Na bila shaka Allah Alimsemesha Musa صلى الله عليه وسلم maneno moja kwa moja”58. Na Allah Alikwishakuwa Mwenye kusema (tokea azali) na wala Hakuwa hivyo kwa kumsemesha Nabii Musa صلى الله عليه وسلم’ 59.
24. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘Qur aani ni Maneno ya Allah ndani ya misahafu yameandikwa, na vifuani yamehifadhiwa, na kwenye ndimi husomwa, na juu ya Nabii Muhammad صلى الله عليه وسلم yameteremshwa’ 60.
56 Fiqhul Akbar, uk.301.
57 Fiqhul Akbar, uk.302.
58 An Nisaa 4:164.
59 Fiqhul Akbar, uk.302.
60 Fiqhul Akbar, uk.301.
32
25. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘Na Qur aani (ni Maneno ya Allah) na si mahuluku’ 61.
61 Fiqhul Akbar, uk.301.
33
Kauli za imamu Abu Hanifa kuhusu Qadar
1. Alikuja mtu kwa imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) akimjadili kuhusu Qadar62, imamu Abu Hanifa akamwambia: ‘Je, kwani wewe bado hujaelewa kuwa mwenye kutazama kwenye Qadar ni sawasawa na yule mwenye kutazama kwenye jua kwa macho yake mawili, kila akizidi kutazama ndio huzidi kuchanganyikiwa’63.
2. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa64: ‘Allah Alikuwa Mjuzi kwa vitu (vyote) toka azali kabla ya hivyo vitu kuwa (kuumbwa) kwake’65.
62Mfasiri: Kuamini Qadar hakutotimilia mpaka pale yatakapokusanyika ndani ya moyo wa mja mambo manne:
i. Kuamini kwamba Allah ni Mjuzi Pekee wa kila kitu kwa ujuzi uliosabiki.
ii.Kuamini kwamba Allah Ameandika makadirio ya kila kitu kwenye Lawhil-Mahfuudh (Ubao uliohifadhiwa).
iii. Kuamini kwamba hakiwi chochote kile si ardhini na wala si mbinguni isipokuwa kwa Irada ya Allah na kwa Matakwa Yake.
iv. Kuamini kwamba kila kitu ardhini na mbinguni ni mahuluku wa Allah; havina Muumba pasina Yeye na wala havina Rabi asiyekuwa Yeye. Angalia, Sharhu Thalathatil Usul cha Ibn Uthaymiyn (Rahimahullahu).
63 Qalaid uqudil aqyan (q-77-b).
64 Fiqhul Akbar, uk.302-303.
65 Mfasiri: Hili linathibitisha Ujuzi (Elimu) ya Allah kama ilivyothibiti kwenye Hadithi:
عَنْ عَبْ ه د اللََّّه بْ ه ن عَمْ ه رو بْ ه ن الْعَا ه ص رَ ه ضيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ سَ ه معْتُ رَسُولَ اللََّّه صلى الله عليه وسلم
يَقُولُ : " كَتَبَ اللََُّّ مَقَا ه ديرَ الْخَلاَئه ه ق قَبْلَ أَنْ يَخْلُقَ السَّمَوَا ه ت وَالْرَْضَ بهخَمْ ه سينَ
أَلْفَ سَنَةٍ قَالَ وَعَرْشُهُ عَلَى الْمَا ه ء " . - -
Kutokana na Abdillah bin Amru (Allah Awe Radhi Nae) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم akisema kuwa: “Allah Aliandika Makadirio ya viumbe miaka elfu hamsini kabla ya Kuumba mbingu na ardhi - akasema -: Na Arshi Yake (ilikuwa) iko juu ya maji.” Muslim, katika Kitabu cha Qadar (Kadari), mlango wa Mjadala Kati ya Adam na Musa (Amani Juu Yao). Hadithi namba (6416).
34
3. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘Allah Anamjua asiyekuwepo katika hali ya kutokuwepo kwake huyo asiyekuwepo, na (Allah) Anajua hakika vipi atakuwa hapo Atakapomfanya kuwa, na Allah Anamjua aliyekuweko katika hali ya kuweko kwake huyo aliyekuweko, na Anajua vipi itakavyokuwa kutokuwapo kwake’66.
4. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘Qadar Yake (imeandikwa) kwenye Ubao uliohifadhiwa’ 67.
5. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa68: ‘Na tunakiri kuwa Allah Aliiamuru kalamu kuandika, kalamu ikasema: Niandike nini ewe Rabbi?! Allah Akasema: Andika yale yote yatakayokuwa mpaka Siku ya Qiyamah69, kwa Kauli Yake:
66 Fiqhul Akbar, uk.302-303.
67 Fiqhul Akbar, uk.302. Angalia note namba 62.
68 Waswiyyah pamoja na ufafanuzi wake, uk. 21. 69 Mfasiri: Kitu cha kwanza kilichoumbwa na Allah kilikuwa (ni) kalamu; Akaiambia andika makadirio ya viumbe vyote hadi itakaposimama Qiyamah: عَنْ أَبهي حَفْصَةَ، قَالَ قَالَ عُ بَادَةُ بْنُ الصَّا ه م ه ت رضي اللهُ عنه ه لابْنه ه يَا بُنَىَّ إهنَّكَ
لَنْ تَ ه جدَ طَعْمَ حَ ه قيقَ ه ة ا ه لإيمَا ه ن حَتَّى تَعْلَمَ أَنَّ مَا أَصَابَكَ لَمْ يَكُنْ ه ليُخْ ه طئَكَ وَمَا
أَخْطَأكََ لَمْ يَكُنْ ه ليُ ه صيبَكَ سَ ه معْتُ رَسُولَ اللََّّه صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " إهنَّ أَوَّلَ مَا خَلَقَ اللََُّّ الْقَلَمَ
فَقَالَ لَهُ اكْتُبْ . قَالَ رَ ه ب وَمَاذَا أَكْتُبُ قَالَ اكْتُبْ مَقَا ه ديرَ كُ ه ل شَىْءٍ حَتَّى تَقُومَ
السَّاعَةُ " . يَا بُنَىَّ إهنه ي سَ ه معْتُ رَسُولَ اللََّّه صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " مَ نْ مَاتَ عَلَى غَيْ ه ر هَذَا
فَلَ يسَ ه منه ي " .
Kutokana na Abu Hafsah (Allah Amrehemu) amesema kuwa; Ubadah bin Swamit (Allah Awe Radhi Nae) alisema kumwambia ibn wake: ‘Ewe mwanangu! Kwa hakika hutaweza kupata uhakika wa ladha ya imani mpaka pale utakapoweza kufikia kuelewa kwamba (chochote kile) kilichokusibu hakikuwa chenye kuweza kukukosa, na kwamba kilichokukosa hakikuwa chenye kuweza kukusibu’; nilimsikia Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم akisema: “Kwa hakika kitu cha kwanza Alichoumba Allah ni
35
وَكُلُّ شَيْءٍ فَعَلُوهُ فهي الزُّبُ ه ر ﴿ ٥٢ ﴾ وَكُلُّ صَ ه غيرٍ وَكَ ه بيرٍ مُّسْتَطَرٌ ﴿ ٥٣ ﴾
“Na kila kitu wakifanyacho kimo katika maandiko (madaftari yanayorekodi amali). Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa”70.
6. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema71: ‘Na wala hakiwi kitu chochote kile duniani na wala Akhera isipokuwa kwa Matakwa Yake.’72
7. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘Allah Ameumba vitu (vyote) si kutokana na kitu chochote kile’73.
8. Na akasema kuwa: ‘Allah Alikuwa Khaaliq (Muumba) kabla ya kuumba chochote.’ 74
kalamu, Akaiambia: Andika. (kalamu ikasema): ‘Niandike nini, ewe Mola wangu! (Allah) Akasema: Andika makadirio ya kila kitu mpaka itakaposimama Saa (Qiyamah)”. (Ubadah bin Swamit Allah Awe Radhi Nae) akasema: ‘Ewe mwanangu! Hakika mimi nilimsikia Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم akisema: “Mwenye kufa juu ya ghairi haya basi (huyo) si katika mimi (si katika umma wangu)”. Abu Dawud katika kitabu cha Sunnah, mlango wa Katika Qadar. Hadithi namba (4683); na Tirmidhi katika Kitabu cha Qadar kutokana na Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم. Hadithi namba (2155). Hili ni lafdhi la Abu Dawud.
70 Al Qamar 54:52-53.
71 Fiqhul Akbar, uk.302.
72 Mfasiri: Aayah hii ni miongoni mwa Aayat nyingi zenye kuthibitisha Matawa na Ujuzi (Elimu) ya Allah: وَمَا تَشَاءُونَ إهلَّا أَن يَشَاءَ اللَّه إۚهنَّ اللَّهَ كَانَ عَ ه ليمًا حَ ه كيمًا ﴿ ٣٠ ﴾
"Na hamtoweza kutaka isipokuwa Atake Allah; hakika Allah daima ni Alimu (na) Hakimu." Al Insani 76: 30.
73 Fiqhul Akbar, uk.302.
74 Fiqhul Akbar, uk.304.
36
9. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Tunakiri kwamba mja pamoja na amali zake (matendo yake) na ikirari (ukubalifu) yake na ujuzi wake ni mahuluku75, basi ilivyokuwa mtenda (mja) ni mahuluku, basi vitendo vyake vinahaki zaidi kuwa mahuluku’ 76.
10. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Vitendo vyote vya waja; kuanzia harakati zao (kutikisika kwake) na kutotikisika kwake ni chumo lao (vinastahiki malipo) na Allah Ndiye Muumbaji Wake (hivyo vitendo vyote), na vyote hivyo ni kwa Matakwa Yake, na Elimu Yake, na Qadhaa Yake na Qadari Yake’ 77.
11. Imamu Abu Hanifyah (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘Na vitendo vyote vya waja; kuanzia harakati zao na kutotikisika ni chumo lao kwa uhakika, na Allah Ameviumba, na vyote hivyo ni kwa Matakwa Yake, na Elimu Yake na Qadhaa Yake na Qadari Yake. Na amali njema zote zimekuwa wajibu kwa Amri ya Allah, na kwa Mahaba Yake, na kwa Ridhaa Yake, na Elimu Yake na Matakwa Yake, na Qadhaa Yake, na Makadiro Yake; na maasi (vitendo vya kumuasi Allah) yote (hutokea) kwa Elimu Yake, na Qadhaa Yake, na Makadirio Yake na Matakwa Yake, na wala sio kwa Mahaba
75 Mfasiri: Aayah hii ni miongoni mwa Aayat zenye kuthibitisha kuwa mja na matendo yake ni mahuluku:
وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَ ا تَعْمَلُونَ ﴿ ٩٦ ﴾
"Na Allah Amekuumbeni (nyinyi) na (pia Ameyaumba) yale mnayoyafanya." Asw-Swaaffaat 37: 96.
76 Waswiyyah pamoja na ufafanuzi wake, uk.14.
77 Fiqhul Akbar, uk.303.
37
Yake, na wala sio kwa Ridhaa Yake na wala sio kwa Amri Yake’78.
12. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Allah Ameumba viumbe hali ya kuwa ni wenye kusalimika na kufuru na imani79, kisha Akawahutubia na Akawaamrisha na Akawakataza; basi alikufuru yule aliyekufuru kwa kitendo chake cha kukataa na kukanusha kwake haki, kwa hivyo Allah Alimuachia (kupotoka kwa kuwa mwenyewe alitaka hivyo); na aliamini yule aliyeamini kwa kitendo chake cha ikirari na kusadikisha kwake na kwa Taufiki ya Allah na Nusra ya Allah kwake’80.
13. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘(Allah) Aliwatoa dhuria wa Adam kutoka kwenye mgongo wake (Adam) katika sura ya atomu, Akawajaalia wenye akili, kisha akawahutubia na Akawaamrisha imani na akawakataza ukafiri. Basi walikiri Uungu (Uola) Wake; hiyo ikawa kutoka kwao ndio imani, basi wao wanazaliwa juu ya fitwrah (umbile la kuelemea kwenye kumpwekesha Allah); na yeyote yule aliyekufuru amekufuru baada ya hayo, basi bila shaka huwa amegeuza na kubadilisha; na yeyote yule aliyeamini na akasadikisha, basi huwa amethibiti juu yake na amedumu nayo’ 81.
14. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na Yeye Ndiye Ambaye Amekadiria vitu (vyote) na Akavikidhia,
78 Fiqhul Akbar, uk.303. 79Kilichosahihi ni kuwa: Allah Ameumba viumbe juu ya fitwrah (umbile la kuelemea kwenye kumpwekesha Allah), kama atakavyokuja kubainisha imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) kwenye kauli ifuatayo.
80 Fiqhul Akbar, uk.302-303.
81 Fiqhul Akbar, uk.302.
38
na haliwi lolole lile duniani na wala katika Akhera isipokuwa kwa Matakwa Yake, na Elimu Yake, na Qadhaa Yake, na Qadari Yake, na (yote haya) Ameyaandika kwenye Ubao uliohifadhiwa’82.
15. Imamu Abu Hanifa (Rahimahullahu) amesema: ‘Allah Hakumlazimisha mmoja yeyote yule katika viumbe Vyake kukufuru na wala kuamini, bali Aliwaumba kama ni watu, na imani na kufuru ni matendo ya waja. Na Allah Anamjua yule atayekufuru katika hali ya kukufuru kwake hali ya kuwa kafiri, na atakapokuja kuamini baada ya hapo na kuwa ni Muumini Atampenda bila ya kubadilika Elimu Yake’ 83.
82 Fiqhul Akbar, uk.302.
83 Fiqhul Akbar, uk.303.
39
Kauli za imamu Abu Hanifa Kuhusu Imani
1. Imamu Abu Hanifa (Rahimahullahu) amesema kuwa: ‘Imani ni ikirari na kusadikisha’ 84.
2. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema kuwa: ‘Imani ni ikirari kwa ulimi na kusadikisha kwa moyo, na ikirari peke yake haiwi imani”85. Ameinukuu Twahawi (Allah Amrehemu) kutoka kwa Abu Hanifa na sahiba zake wawili (Allah Awarehemu)’86.
3. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Imani haizidi wala haipunguwi’87. Nikasema (Mtungaji): Kauli yake (hii) katika kutozidi kwa imani na kutopungua kwake na kauli yake katika kile chenye kuitwa imani kuwa ni kusadikisha kwa moyo na ikirari kwa ulimi, na kwamba amali ziko nje na kile chenye kuitwa uhakika wa imani. Kauli yake hii ndio yenye kudhihirisha tofauti baina ya itikadi yake [imamu Abu Hanifa Allah Amrehemu] katika imani na baina ya itikadi ya maimamu wengine wa Kiislamu: Malik, na Shafi, na Ahmad, na Ishaaq, na Bukhari, na wengineo; na haki iko pamoja na hawa maimamu (Allah Awarehemu Jamia); na Abu Hanifa (Allah Amrehemu) hakusibu, na yeye ni mwenye kupata ujira kwa hali mbili, na Ibn Abdul Barr na Ibn Abil Izzi wametaja yale yenye kuonyesha kuwa imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) aliachana na kauli yake na Allah Anajua Zaidi 88.
84 Fiqhul Akbar, uk.304.
85 Waswiyyah pamoja na ufafanuzi wake, uk.2.
86 Twahawiyyah, na ufafanuzi wake, uk.360.
87 Waswiyyah pamoja na ufafanuzi wake, uk.3.
88Tamhid cha Ibn Abdul Barr 9/247, ufafanuzi wa Aqidatutw Twahawiyyah, uk.395.
40
Kauli yake kuhusu Swahaba
(Allah Awe Radhi Nao Jamia)
1. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na wala hatumdhukuru mmoja yeyote yule miongoni mwa Swahaba wa Rasuli wa Allah (Allah Awe Radhi Nao Jamia) isipokuwa kwa kheri’ 89.
2. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na wala hatumtengi (hatujiweki mbali na) mmoja yeyote yule miongoni mwa Swahaba (Allah Awe Radhi Nao Jamia) wa Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم na wala hatumfanyi mmoja yeyote yule miongoni mwao kuwa ni rafiki kipenzi pasina mmoja mwengine’90.
3. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Ukaaji wa mmoja wao pamoja na Rasuli wa Allah صلى الله عليه وسلم kwa saa moja tu ni bora kuliko amali za mmoja wetu umri wake wote na hata ukiwa mrefu vipi’ 91.
4. Imamu Abu Hanifa (Allah Amrehemu) amesema: ‘Na tunakiri kuwa mbora wa umma huu baada ya Nabii Muhammad صلى الله عليه وسلم ni Abu Bakr (Allah Awe Radhi Nae), kisha Umar (Allah Awe Radhi Nae), kisha Uthman bin Affan (Allah
89 Fiqhul Akbar, uk.304.
90 Fiqhul Absatw, uk.40.
91 Manaqib Abi Hanifa cha Al Maliky. uk.76.

 

 

bottom of page