Tuna Haja ya kuwatayarisha Maulamaa Zanzibar
Hivi karibuni nilibahatika kutembelea visiwa vya Zanzibar, visiwa vilivyokuwavikieleweka na kusifika kuwa ni kitovu na kitivo cha elimu na ustaarabu kwakaribu eneo lote la mwambao na bara ya mashariki ya Afrika, nilitembelea wakati nikiwa katika siku za mapumziko.
Kwanza sina budi kutanguliza shukurani zangu za dhati kwa wale ninaowalenga ambao ni Waislamu na wanaharakati wa Kiislamu kwa kuona maendeleo yanayoridhisha katika suala zima la Da’awah. Kwani darsa zinaendelea na kushamiri kwa kule kuwepo kwake yapo kwa wingi, kadhalika kwa upande wa Mihadhara nayo pia inafanyika, makongamano ya Kiislamu yenye kuwasilishwa ndani yake mada zenye maudhui tofauti pia yanaandaliwa ikiwa ni juhudi miongoni mwa juhudi jabari za kuuhuisha na kuuendeleza Uislamu katika visiwa vyetu hivyi.
Pia kuwepo kwa taasisi za Kiislamu ambazo zimeweza kufikia kumaizi(kutambua) nini majukumu yake, na kujaribu kuyatekeleza kadiri ipasavyo katikakuijenga, kuitayarisha na kuielimisha jamii kielimu, kimaarifa na kimaendeleo yenye kwenda na wakati, na wakati huohuo kuizindua na kuitanabahisha kwa kuitahadharisha katika yale ambayo ni wajibu kwa Waislamu kutahadharishana.
Mafanikio haya inawezekana yakawa si rahisi kwa mkaazi kuweza kufikia kuyatambua wachilia mbali kuyaona kama ni mafanikio, lakini kwa yule asiyekuwa mkaazi mwenye fungamano na mambo kama haya, huwa na shauku ya kuona wafanyavo wengine, huwa na hamu ya kufuatilia mbinu, taratibu na njia wanazozitumia, na mwisho kudadisi hatua waliyoweza kuchukuwa na kufikia, na matatizo waliyokutana nayo, basi kila akipata fursa ya kwenda na kujionea mabadiliko ni jambo la kuridhisha sana.
Hata hivyo kuna jambo ambalo kulingana na upeo wangu mdogo ni la kushitua.Jambo lenyewe ni kule kuweza kufikia kugundua kuwa baadhi ya wahadhiri na walimu wenye kuhadhiri na kusomesha kwenye baadhi ya madarsa na kutoa mihdhara kuwa wamefikia kunasibishwa na Maulamaa, bali hata kwa wengine kupewa daraja ya kuwa ni miongoni mwa wanazuoni.
Kuwa mwanachuoni (Aalimu) na kuwa ni mwalimu ni daraja mbili tofauti.
Mwalimu ni kila anaefundisha na kuelimisha wengine elimu au maarifa fulani, iwe katika madarsa au maskuli, na sehemu nyengine zozote zile zenye kueleweka kuwa ni zenye kutoa elimu. Ama Aalimu ni (Mwanazuoni) ni yule pekee aliyebobea na kutabahari katika elimu, ni yule mwenye utaalamu wa kiwango cha juu cha somo au maarifa katika fani yake kwa kuwa miongoni mwa majukumu yake ni kule kufikia kuweza kutaamali na nususi kwa kuzifafanua, na kuzielezea, kuzifanyia tafiti za kielimu, na kubwa ambalo kwa wengine ni muhimu na ndio hasa lenye kupelekea mtu kuitwa au kupewa daraja ya Aalimu ni kule kuweza kufikia kuwa na uwezo wa kutunga na kuandika vitabu na kuchapisha tafiti, tafiti ambazo amezichapisha kwa kusudio la kuchambua na kufafanua suala moja katika/miongoni mwa masuala yenye utata kwa kutumia ule utaalamu, ujuzi na maarifa aliyotunukiwa.
Tafiti hizi kwa kawaida hutarajiwa kuwekwa kwenye majarida ya tafiti mbalimbali za taaluma katika vyuo vikuu kwa lengo la kuwepesishia wale wenye kutafiti kuweza kufikia kunufaika na tafiti hizo.Kitu ambacho ninaweza kudiriki kusema kwa uoni wangu wa karibu (mnaweza kunisahihisha nikikosea) ni kwamba suala la uandishi ni dogo na finyu mno tena,suala ambalo ni muhimu sana kwa wanazuoni, wanaharakati na walinganiaji kwa kuwa uandishi ni moja katika Jihaad inayotakiwa kuwepo hai thabiti na yenye nguvu katika jamii kwa kule kuweza kusaidia kuwarudi na kuwajibu kila wenye ukosefu wa elimu na maarifa kuhusiana na Dini, au kuwaweka sawa kila wenye ukosefu wa ufahamu sahihi na kutoelewa suala zima la Dini lenye kuwataka watu kuwa kustahamiliana na kuishi bila ya kulazimisha katika kufuata dini.
Hii ni kusema kuwa uandikaji, utafiti (masuala ambayo yalipewa umuhimu na wanazuoni waliotangulia), na likijumuishwa pia suala zima la uchapishaji hayapo au ni finyu mno tena hasa kwa wale wanaoonekana na kutegemewa kuwa niwanazuoni katika jamii yetu.
Kwa uoni wangu ni kuwa jambo hili halipo au limekosekana, na bila shaka yoyote ile kuna sababu zilizopelekea kufikia hali hiyo; na huenda ikawa mojawapo ya sababu hizo ni ile yenye kufungamana na wanaharakati, kuwa wengi miongoni mwao bado hawajaweza kufikia kuuona au kuelewa umuhimu wa kuandika maudhui katika Dini hasahasa zile zenye mijadala mikali na mivutano isiyomalizika inayopelekea kufarikisha na kutatiza jamii.
Ni vyema tuelewe kuwa kukosekana kwa uandishi au tafiti katika maudhui kama hayo katika jamii hupelekea kupatikana kwa madhara mengi; yakiwemo yale yenye kufungamana na elimu ya mwanazuoni, kwani kuondoka kwake duniani huwa ndio kuondoka au kupotea kwa ile elimu yake isipokuwa sehemu chache iliyodhibitiwa kwa njia ya kupokelewa na wanafunzi wake.
Miongoni mwa misiba mikubwa ni kule kuondokewa na Aalimu aliye mifano wa kuigwa, na katika shida kubwa kabisa na yenye kuhiliki ni kule kuhiliki kwa Aalimu Ar Rabbaniy1, na katika kuchakaa ni kufa kwa Aalimu wa Qur-aan mwenye mpasuko kwa usomaji kwa Qur-aan na huku dunia ikiwa na kiu juu yake na elimu yake na kukosekana wa kujaza pengo aliloliacha kwa jamii.
Ukweli ni kuwa moja katika Sunnah za Allah ni kuwa Huiondosha elimu kwa watu pamoja na kule kufa kwa mwanazuoni Ar Rabbaniy, kama ilivyothibiti katika Hadithi ya Abdullahi bin Amru (Radhiya Allahu ‘anhu),ِ
Amesema „Abdillaah bin Amru (Radhiya Allahu ‘Anhuma) amesema:Nimemsikia Mtume wa Allah (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi waaalihi waSallam) akisema: “Hakika Allah Haichukui elimu (kutoka vifuani mwa watu) kwa kuing‟oa baada ya Kuwapa, lakini Huichukua (kutoka vifua vya wanazuoni) pamoja na kuwafisha wanazuoni na elimu zao, basi watabakia watu majahili wanaulizwa (wanaombwa kufutu juu ya masuala ya Dini), basi watatoa fatuwa bila ya ujuzi, watapotea (wao wenyewe) na wanapoteza (watu wengine)”
Huo ndio msiba na janga la uhakika, lau kama elimu yake ameiandika na kuichapisha au hata bila ya kuichapisha, lakini iko pahala fulani imedhibitiwa, basi faida isiyokadirika ingewafikia na kuwanufaisha wengi.Pia huenda sababu ikawa ni ile yenye kufungamana na kipato cha mwanachuoni,au kwa jamii kutoshajiika au kutoona umuhimu suala la kudhamini wanazuoni na uchapishaji wa kazi zao kutokana na ughali wa gharama za uchapishaji, au kutokuwepo utamaduni wa kusoma vitabu katika jamii na kadhalika. Jambo linalopelekea kwa wengi kutofikiria kutafiti wachilia mbali kuandika, kwani lengo kuu la kutafiti (kwa dhana ya wengi) na kuandika ni kufikia kuweza kuchapishwa ili waje kunufaika wale wataokuja baadae.
Hivyo basi mtu wa kawaida huonavigumu kujiingiza katika kazi ambayo hatima yake haieleweki.1
Allah Anasema:ْ Bali: Kuweni wanazuoni rabbaniyyiyna kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yalemliyokuwa mkiyadurusu.” Aal „Imraan 3:79.
Kusudio la wanazuoni rabbaniyyiyna ni wale watekezaji kulingana na elimu yao waliyotunukia na Allah, au wanazuoni wenye kuwalea na kuwafundisha watu yale waliyoyasoma na kudurusu kutoka kwenye Kitabu ya kumpwekesha Allah katika kila chenye kumuhusu Yeye, au mwanazuoni mwenye kufundisha watu hatua kwa hatua; kwa kuanza cha kwanza na kidogo kidogo mpaka kufikia kiwango cha juu. 2Bukhaariy, katika Kitabu cha Kushikamana na Kitabu na Sunnah, mlango wa yale yenye kudhukuriwa katika kulaumu rai ….
Nukta hii kwa wengi wetu yawezekana tukaiunga mkono na kuiona kuwa ina mantiki hasahasa kwa kuwa tuko kwenye zama zenye mitandao ambayo hutumiwa karibu na wengi wetu. Hii ni kusema kuwa katika ulimwengu wetu wa leo kazi zinazofanywa au zitazofanywa na walengwa zingeweza kunufaisha na kufaidisha wengi, kwa kuwa zingeweza kupelekwa na kuwekwa katika tovuti za Kiislamu –kama inavyodhaniwa na kutarajiwa na wengi- kama ni kianzio ambacho kingeweza kushajiisha wengine wengi, na kupelekea kuleta changamoto tofauti zikiwemo zile za katika kuhoji na za kutolewa maelezo, na za ufafanuzi hasahasa kwa wanaotembelea tovuti hizo ambazo licha ya jitihada za kuasisiwa bado zinakosa wachangiaji (huenda wakawa hawaelewi kuwa hilo liko, na linakaribishwa) ambao tunaamini kuwa wako na wanao uwezo wa kuandika mengi yanayohusiana na Dini yetu.
Tuchukulie mfano wa mwanachuoni katika wanazuoni waliosabiki ambae ni mashuhuri na ana heshima ya namna yake katika kila pembe ya ulimwengu wa Kiislamu, kwa vitabu vyake ambavyo hutumiwa na kutumika na makundi mbalimbali na yenye mitazamo tofauti; mwanachuoni mwenyewe ni Imaamu AnNawawiy (Allah Amrehemu).Imaam Muhiyyid Diyn Abu Zakariya Yahya bin Sharaf An Nawawiy aliyefariki akiwa na umri wa miaka 45 (Allah Amrehemu). Lakini juu ya kufariki kwake na hali ya kuwa ni kijana , zile kazi zake alizoziacha katika maandiko ni za kupigiwa mfano, kiasi cha kwamba nyingi ndizo zinazotegemewa katika mitaala ya ufundishwaji katika taasisi za kielimu za Kiislamu nyingi ulimwenguni.
Kazi zake hazikutumiwa kama ni bahati tu, bali ni kwa sababu ya mfumo wake wa uandishi na uhakiki mpaka zimeweza kukubalika na kuheshimika takriban kwa karne nane tokea kufariki kwake, na zitaendelea kutumiwa na kutumika hadi Atapoirithi Allah ardhi na waliomo ndani yake.
Pia tuchukuwe mfano mwengine, mfano wa mwanachuoni katika jamii yetu aliyetangulia pia, ambae ni mashuhuri na pia ana heshima ya namna yake katika kila pembe ya Afrika mashariki, kwa vitabu vyake ambavyo hutumiwa na kutumika na wengi, mwanachuoni mwenyewe ni Sheikh Abdullah Swaleh AlFarsy (Allah Amrehemu).
Sheikh Al Farsy (Allah Amrehemu) aliheshimika katika enzi za uhai wake na anaendelea kuheshimika baada ya kufariki kwake, na si kwa elimu yake tu, bali anaenziwa pia kwa kazi zake za uandishi, kazi ambazo wengi waliokuwa hawamfahamu vizuri wameweza kumjua vizuri kwa ujumla kwa kupitia vitabu vyake alivyoviandika, na kwa ile Tafsiri yake ya Qur-aan katika lugha ya Kiswahili hususan.
Sh Al Farsy (Allah Amrehemu) alikuwa ni mtetezi wa Sunnah katika enzi zake,lakini wengi hawakuweza kumuelewa au walimuelewa lakini walikuwa katika hali ya kugubikwa na hali ya jamii iliyokuwepo. Kwa wale waliobahatika kuzisikiliza kanda zake za mawaidha katika siku hizi wanafaidika vyema na mafundisho ambayo wengi katika siku hizi wanadai kuwa ni mageni na kwamba hayakuwahi kusemwa na wanazuoni waliopita lakini ukweli ni kuwa Sh Al Farsy aliyasema na aliyatanabahisa miaka mingi iliyopita.
Binafsi nilibahatika kuandika kitabu cha Mirathi mwaka 2002. Chimbuko lake lilikuwa ni mkusanyiko wa durusu zilizokuwa zikifanyika katika Masjid AlFalaah, Mombasa hapo Zanzibar.Kwa hakika hii njia ya kukusanya durusu, mihadhara, makala na kadhalika,walisabiki katika hilo wanazuoni wetu waliotangulia, kwani Sh. Al Farsy (AllahAmrehemu) ameweka wazi katika utanglizi wa tafsiri yake kuwa; katika mwezi wa mfungo nne, mwaka 1370 sawa na Octoba, 1950 alianza kwa kutabiisha: Sura za Sala na tafsiri zake; kisha Tafsiri ya baadhi ya sura za Qur-aan … kisha akaanzisha mpango wa kutoa tafsiri ya juzuu moja moja…. Mpaka akamaliza tafsiri ya Quraan nzma.
Hivyo basi huu utaratibu wa kukusanya durusu, mihadhara. makala, na kadhalika,ni utaratibu mzuri na ni wa kuigwa na walengwa, kwani unaweza kumsaidia mhusika wake kwa kile alichokikusanya kuweza kufikia daraja ya kuandikwa na kuchapishwa, au hata kufanyiwa tafiti; kwani wanazuoni waliotangulia walikuwa wakiandika makala kwa mikono yao na hawakuwa na uwezo wa kuchapisha, na baadae wakaja watafiti na kutafiti kilichoandikwa na kupelekea kuchapishwa vitabu vyenye kutumiwa na kunufaisha.
Hii ni mifano michache itakayoweza kukupa taswira ya hadhi ya uanazuoni ambayo inaakisiwa zaidi kwenye uandishi ikiwa ni kama kumbukumbu ya kazi zilizofanyiwa kazi na kupitiwa, kuhakikiwa, na kufanyiwa tafiti, na kisha kuchapishwa na kubaki kama Sadaqatun Jaariyah.
Kigezo cha kuwa Aalimu ni daraja ya juu katika mizani ya kielimu, hivyo basi tutumie istilaahi hii na kuinasibisha kwa wale wenye kustahiki kunasibishwa nayo.
Hapa nitapenda na kutoa mfano mmoja wa mtafiti wa mambo ya Kiislamu, mtafiti huyu alipotembelea Zanzibar jambo la kwanza alilotaka lilikuwa ni kupelekwa kwenye duka la vitabu vya Kiislamu, hakutaka kupelekwa kwenye vyuo vikuu au kwenye taasisi za Kiislamu au kukutana na wanaharakati au wahadhiri wa Kiislamu au walinganiaji wake, bali alichotaka kilikuwa kupelekwa pahala ambapo karibu hawa wote hutarajiwa kupatembelea na kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na wa pekee napo, pahala ambapo mtu ataweza kukutana na makala, majarida, magazeti,tafiti, rejea na vitabu vya Kiislamu.
Mtafiti aliomba na kusisitiza kupelekwa huko kwa ajili ya kupata kuiona hali halisi ya Waislamu wa visiwa hivi na namna walivyojizatiti katika suala la kuhuisha na kuendeleza Dini kwa kupitia njia inayofunganisha baina ya waliotangulia na wajao ambayo ni njia ya Uandishi.
Kilichomsikitisha ni kuwa hakukutana na kazi yoyoteile ambayo inaweza kufikia kuitwa kazi ya kitaaluma katika vitabu vichache vinavyouzwa kwenye maduka ya vitabu vya Kiislamu vilivyoandikwa katika lughaya Kiswahili.
Jambo hili tu linaweza kutupa taswira halisi ya suala zima la uandishi miongoni mwa mashekhe, wahadhiri, watafiti na huenda likawagusa pia wanaharakati wakida’wah.
Mtihani wetu si kwenye uandishi pekee, bali hata kwenye wahusika wa harakati zada’wah za Kiislamu, kwani wengi wao huwa bado wanategemea akili zao badala ya maandishi katika kudhibiti na kuhifadhi matukio na taarifa mbalimbali za kitaalamu zenye kufungamana na da’wah na mwenendo wake, kwa sababu moja au nyengine, wakisahau kuwa akili huwa dhaifu kila umri ukisonga mbele, jambo linalopelekea kupoteza na kupotea kwa taarifa nyingi muhimu.
Kwa mara nyengine binafsi nikiwa miongoni mwa wahusika nakumbuka mwaka 2008, nilipokuwepo Zanzibar, nilibahatika kukutana na mwanaharakati mmoja ambae alinisimulia kisa cha kijana mmoja wa Kijerumani aliyekuwa akifanya shahada ya uzamili katika athari za da’awah katika visiwa vya Zanzibar. Hii ndio ilikuwa maudhui ya risala/tasnifu aliyoifanyia utafiti.
Kwa mujibu wa mwanaharakati, ili utafiti wa ukamilike na uweze kufikia kubeba hadhi ya risala/tafiti za shahada ya uzamili, kijana huyu katika utafiti wake alihitaji kukutana na watu maalumu ili aweze kuwahoji na kuwadadisi, jambo litaloweza kumsaidia kuweza kufikia kukamilisha kazi yake kwa utaratibu wa kukusanya data(mambo ya hakika au yaliyokubaliwa kuwa hakika) alizozihitajia.
Kilichojitokeza ni kuwa ilikuwa ni mtihani mgumu kuweza kupata mtu mmoja wachilia mbali watu waliokuwa wakitakiwa, watu wenye maarifa na taarifa maalumu ili kupata kukusanya hizo data na vielelezo vyenye kukubalika, ilikuwa vigumu kwa kukosekana watu wenye sifa na vigezo kwa mujibu wa utafiti wake jinsi alivyoupanga.
Badala yake alilazimika kuwasiliana na watu ambao kwa mtazamo wa kijuujuu hudhaniwa kuwa ndio wenye sifa za kuweza kuelezea hali halisi ya da’awah bila ya hata na kuwa na vielelezo timilifu na vyenye kiwango kinachokubalika kitaaluma.
Kwa ujumla wanaharakati wetu wanategemea zaidi uzoefu wao katika kujihusishakwao na harakati za da’awah, badala ya kuwa na utaratibu wa ukusanyaji, uwekaji,na udhibiti wa taarifa kwa kutumia nyenzo za kisasa ambazo zinapatikana.
Zanzibar sasa ina vyuo vikuu vitatu; navyo ni: Chuo kikuu cha Zanzibar (ZanzibarUniversity) kilichopo Tunguu, State University odf Zanzibar (SUZA) naAbdulrahman Al-Sumait University (SUMAIT University) iliyokuwa ikijulikana kama ni University College of Education kilichopo Chukwani, katika taaluma zake kuna pia taaluma yenye kuhusisha fani mbalimbali za taaluma za Dini yaKiislamu; kinachotakikana kushajiishwa na kupewa msisitizo na umuhimu wa juu ni kuweko na taaluma maalumu itayoweza kusaidia kuandaa wakufunzi wataaluma husika kwa lengo la kusaidia kuweza kufikia kuwa wanazuoni wa baadae;hili ni jepesi kutekelezeka kama lilikuwa ni miongoni mwa malengo ya kuasisiwa kwa hivi vyuo vikuu, lakini sidhani kwa vyuo hivi kuwa vitakuwa vimeweka jambo kama hili miongoni mwa malengo ya kuasisiwa kwake; hivyo basi itabakia jukumu hili juu ya ummah wenyewe na wanazuoni na wanaharakati wake.
Nafasi na sifa za wanazuoniInatosheleza katika kubainisha utukufu wa wanazuoni na uzito wa majukumu yao,na umuhimu wake vile Alivyowasifia Allah katika sehemu tofauti katika Kitabu Chake kwa kuwapa sifa maalumu na ni ya pekee na ni muhimu kwao, sifa ya kuwana unyenyekevu na wala hawana khofu lawama za mwenye kulaumu, kuwanyanyua daraja ya juu, na Kutuamrisha kurejea kwao, na pia vile alivyowaelezea Rasuli Wake (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) kuwa ni warithi wa Manabii.
Basi inapotokea fitina, mitihani, misukosuko, na mambo kuparaganyika kwa kuchanganyika baina ya mazuri na mabaya na kupelekea kutoweza kufikia kubaini yaliyo sahihi, na jamii ikahitaji mtengenezaji na muongozaji na ikawa wakati huo hakuna Manabii wa Allah (‘alayhimus Salaam), basi jamii hutakiwa uwakusudie warithi wa Manabii (‘alayhimus Salaam) wenye kusema kwa kauli zao,wajiongoze kwa miongozo yao, na nafasi hii ni ya kipekee kwa wanazuoni, na kama pataulizwa kwa sababu gani, basi jawabu ni Kauli Yake Ta’alaa:ُ
Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaoujua na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu”6.3
Allah Anasema
“Kwa hakika wanaomkhofu Allah miongoni mwa waja Wake ni maulamaa.” Faatwir 35:28.
Allah Anasema
“Allah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu.” AlMujaadalah 58:11
Rasuli wa Allah (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema:
“Na hakika Maulamaa ni warithi wa Mitume. Na hakika Mitume hawarithiwi Dinari wala Dirham,bali wao wanarithiwa elimu, kwa hivyo atakayeipata elimu hiyo amepata bahati kubwa” AbuDaawuud, katika Kitabu cha Elimu, mlango wa kushajiisha/kuhimiza kutafuta elimu.
Amesema imamu Ahmad (Allah Amrehemu): “Himdi zote ni za Allah Ambaye amefanya katika kila wakati, kipindi ambapo Mitume (‘alayhimus Salaam) hawawepo, kunabaki wanachuoni wanamlingania yule aliyepotea katika uongofu na wanavumilia dhidi ya maudhi. Wanahuisha kwa Kitabu cha Allah wale waliokufa na kwacho wanamfanya kuona yule ambaye ni kipofu, na kwa Nuru ya Allah wanamfanya kuona yule ambae ni kipofu. Ni wengi waliyoje waliyouawa na Ibliys wamewahuisha! Ni wapotevu wangapi wamewaongoza! Ni athari nzuri iliyoje walionayo kwa watu, na ni athari mbaya iliyoje walionayo watu dhidi yao…. Tunamuomba Allah atukinge na fitina za wapotevu.
"Wanazuoni wanaokusudiwa ni wale pekee waliorithi elimu na amali; elimu ya kuelewa na kutekeleza katika hali zao zote; iwe hali ya siri na ya dhahiri, na wanashikamana na manhaji yao katika hali ya ghadhabu na ridhaa, na uchangamfu na uchukizi, na wala hawawi kama wale wenye kumuabudu Allah ukingoni, au kama wale wenye kugandamana na dunia na kufuata hawaa zake.
Jukumu la mwanazuoni
Dini imewabebesha wanazuoni jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa kile alichokuja nacho Rasuli wa Allah (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) kinaendelea kubalighishwa na kuwepo katika jamii mpaka pale Allah Atakapoirithi ardhi na viliomo. Hawa ni wanazuoni Ar Rabbaniyyiy na ambao hutarajiwa kuubeba kwa nguvu zao zote mzigo mzito mno wa kuwaunganisha wanazuoni (kwani mchango wa kila mwanazuoni huwa unahitajika) hususan, na kuunganisha baina ya Waislamu kwa ujumla, na kuhakikisha kuwa majukumu mengine waliyobebeshwana Dini yanatekelezwa kulingana na mafundisho sahihi ya Rasuli wa Allah (SwallaAllahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam).
Kwa kuwa jamii ni mjumuiko wa watu tofauti, hivyo basi wanazuoni huwa na jukumu la kuhukumu, kufutu na kutatua yale yenye kuonekana kuwa ni yenye kutatiza jamii kwa sababu moja au nyengine.
Kwa kawaida wanazuoni huwa wanabeba pamoja nao uongofu, na wakati huo huo huwa ndio kizingiti cha jamii kutokana na upotevu na kuhiliki. Waislamu wa pande zote za dunia huwa wanatarajia mengi sana kutoka kwa wanazuoni ArRabbaniyyiyna yenye kutengeneza palipoharibika na kutatizika, na haya si chochote wala lolote kwa warithi wa Mitume ambao ni Ar Rabbaniyyiyna.
Miongoni mwa majukumu ya wanazuoni:
Kufundisha, kupandikiza mafundisho sahihi ya Dini hatua kwa hatua, jambo hili litatumikia kadhia nzima ya kuanda wanazuoni wategemea, kwani tunda hutegemea mbegu iliyopandwa au pandikizwa. Jamii inahitaji kuwa na mtaalam maalumu wa kuweza kusaidia kuwafikisha wanazuoni wake kuwa wanazuoni ArRabbaniyyiyna.
Wakati wowote ule watakapokosekana kwa wanazuoni kama hawa, basi hatari ya kupotea jukumu lao litabainika kwa jamii, kwani pengo la kutokuwepo kwao hakuna ataediriki kuliziba. Hivyo basi ni wajibu kwa wanazuoni kujitokeza kwalengo la kuziba pengo, na kusimamia mambo, kuwa karibu na jamii na wanajamii wake kabla ya kuzuka matatizo, na pia wakati wa hayo matatizo, na wala wasingojea kuwajia fursa hali ya kuwa ni wenye kujikalia kitako. Kwani wakati wowote ule watapojichelewesha kubeba jukumu walilobebeshwa na Dini, basi waelewe kuwa wengine wasiokuwa na sifa husika watajinyakulia fursa yakujibebesha kisichowahusu kukibeba7.
Kufatiisha, jambo hili pia litatumikia kadhia nzima ya kuanda wanazuoni ArRabbaniyyiyna; ni juu ya wanazuoni Ar Raasikhiyna kuwa na desturi ya kufatiisha wale wenye kudai kuwa ni wanazuoni na kudai kuwa wana elimu, na pia kufatiisha wenye kujinasibisha nayo au kujinasibisha na uanazuoni, au kunasibishwa na moja katika mawili hayo, na kubainisha ukweli wao kwa watu na kuhakikisha kuwa wananyimwa nafasi ya kujiingiza katika jumuiya ya wanazuoni kwa udanganyifu.
Kukabiliana na kila mwenye kutaka kudoofisha au kutilia shaka na wasiwasi uaminifu wa jamii kwa wanazuoni wake, ni juu ya wanazuoni Ar Raasikhiyna kujiweka tayari kukabiliana kwa njia munasaba na kila mwenye kuwapiga vita kwanjia moja au nyengine, kwani lengo lao huwa si wanazuoni, bali ni kuporomosha ule uaminifu wa jamii kwao ambao huwachukiza na kuwakirihisha, hivyo hufanyakila waliwezalo kuweza kufikia kujaribu kuporomosha hadhi hiyo na kudhoofisha uaminifu uliopo baina ya jamii na wanazuoni wake.
Kubainisha majukumu ya kila mwana jamii kulingana na mafundisho ya Dini, ni juu ya wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna kuweka wazi majukumu ya kila pande yenye kuhitajiwa na jamii -viongozi na raia- na kubainisha umuhimu wa kuyatekeleza na wakati huohuo kutahadharisha hatari ya kutotekelezwa na kila mhusika katika usalama, mshikamano, na uhai wote wa jamii, pamoja na hilo mwanazuoni hatarajiwa kujitenga na jamii, bali ni katika majukumu yake kuwa na mawasiliano mazuri na ya karibu zaidi na jamii kwa kuwalingania ulinganio wa Wajumbe wa Allah (‘alahimus Salaam) na kuwatakia rehema ya Mwenye kurehemu.
Kusahihisha na kurekebisha, ni jambo la msingi kuelewa kuwa kukosa, na kukosea au kwenda kombo ni katika maumbile ya mwanadamu Wenye msingi madhubuti katika elimu. kusema kuwa wanazuoni ni ma’swuumiyna), hivyo basi panapotokea hayo panatakiwa kusahihishwa au kurekebishwa kunakokwenda sambamba na mafundisho sahihi ya Dini, na hakuna wenye kuweza kulifanya hilo isipokuwa wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna.
Kuhukumu na Kupatanisha baina ya wanaohasimiana na kugombana au kuvutana au kuhitalifiana, kutofautiana; kutokea hitilafu, au tofauti ni maumbile yakila jamii, lakini kukosekana waamuzi au wapatanishi wasiopendelea upande wowote huwa ni tatizo kubwa, na hakuna anaeweza kuwa mpatanishi au muamuzi wa hayo isipokuwa wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna, kwani hutarajiwa kushikamanana uadilifu kutokana na yale waliyoyasoma na kudurusu katika Kitab.
Kufanya jihaadi kwa kalamu na lisani, ili kuweza kuondosha na kufuta firka,mawazo, itikadi, na tamaduni zenye kusimama kama ni vizingiti katika njia yakuweza kufikia na kupandikiza mafunzo sahihi ya Dini, wanazuoni hutarajiwakulibeba jukumu la kuandika, kufasiri vitabu (ambalo ni finyu katika jamii yetu),kudurusisha na kufundisha kutokana na yale waliyoyasoma na kudurusu katika Kitabu, kwa kufanya hilo huwa ni wenye kufanya Jihaad kwa kalamu (maandishi,tafiti, vitabu na kadhalika) zao wakijumuisha lisani zao.
Kuelewa matukio na matatizo ambayo yanaisumbuwa jamii na kuyatafutia utatuzi ufaao wenye kwenda sambamba na wakati na wenye kufungamana na mafundisho sahihi ya Dini. Wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna katika majukumu wanayotarajiwa kuyatekeleza, hutakiwa kwanza wawe na elimu, ujuzi, na ufahamu mpana na wa kina wa umbile la matukio yanayotokea katika jamii anayoishi nayo,kisha kuwa na elimu ya hukumu ya Dini, ambayo atahukumia kwayo tukio husika. Hizi ni elimu za namna mbili ambazo zinafungamana na wanazuoni ArRabbaniyyiyna: Elimu ya kuelewa tukio, na pia huenda kukahitajika kuelewa sababu za kutokea kwake, na elimu ya kuelewa Hukumu ya Allah inayowajibika kupitishwa au kutolewa kwa hilo tukio.
Kutatua matatizo ya Waislamu katika jamii, hili ndio jukumu linaloonekana kirahisi na kila mwanajamii mwenye macho na hisia ya kuwepo wanazuoni katika kila pande ya ulimwengu wa Kiislamu. Tukichukulia mfano wa haya maradhi yaliyoisibu dunia, maradhi yaliyopelekea kufungwa misikiti, pahala ambapo Waislamu huwa hawako tayari kupakosa mara tano kwa siku, kwa kutekeleza Sala za Fardhi, na hasahasa siku ya Ijumaa hata wasiokuwa na kawaida ya kuswali huwa wanajumuika kwa hilo, lakini limekosekana kutokana na maradhi yenye
Allah Anasema:ِس ُطُاقَْْذ ِل ََأعَِْالٍَُما بْصِل ُحُا بَْيىَۗ ِس ِطي َه﴿ َفَأُمقْْـًَ يُ ِح ُّب الههن اللِإ
٩﴾“ …. basi suluhisheni baina yao kwa uadilifu, na timizeni haki. Hakika Allaah Anapenda wanaotimiza haki” Al Hujuraat 49:9.
Wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna kwa kupitia mafundisho sahihi ya Dini waliweza kufikia utatuzi wa tatizo lililoonekana kuwa ni usumbufu kwa wengi walikuja na fatuwa ya kuwa watu wanaruhusika kuswali majumbani mwao, kulingana na mafundisho sahihi ya Dini yenye kufungamana dalili sahihi.Kufutu masuala yenye kuleta mifarakano na migongano katika jamii, hili nijukumu pevu, jukumu ambalo kwa kweli hakuna awezae kulitatua au kulifutu isipokuwa Wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna.
Kuna masuala mengi yenye kupelekeaWaislamu kufarikiana, kugombana, kutengana, kuhasimiana, na kadhalika, utatuziwake uko kwenye mikono ya Wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna.Kubainisha kwa Waislamu fitina zinazowalenga katika jamii yao hususan, na katika ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla. Wanazuoni hutarajiwa kuwawekea wazi Waislamu fitina au mizizi ya fitina kulingana na mafundisho sahihi ya Dini,katika huku kubainisha hayo Wanazuoni hukadimisha kumridhisha Allah mbele yakumridhisha mja yeyote yule, yote kwa kuwa anapopitisha jitihada huwa lengolake ni kutafuta Wajihi wa Allah na kuhakiki Akitakacho kulingana na Sheria.
Hayo ni baadhi ya majukumu ya mwanazuoni mwenye kutaraji kukutana na Rabi wake kwa jamii yake anayotarajiwa kuielekeza na kuiongoza na kuwa kigezo kwenye yale yote yenye kumridhisha Allah.
Namna ya kuandaa na kutayarishi wanazuoni
Ukweli ni kuwa kuandaa watu wa kawaida kwa kazi za kawaida za kila siku si changamoto ndogo, wachilia mbali unapotaka kupendekeza namna ya kuandaa na kuwatayarisha wanazuoni jambo ambalo ni la wajibu juu ya jamii, hiyo huwa ni changamoto ya aina yake pekee, hasa kuandaa watu waliosifiwa kwa sifa mahususi, sifa ya kumukhofu Allah, sifa itayopeleka kuweza kufikia kuhakikisha kuwa kunapatikana mwanazuoni Ar Rabbaniyyiyna.
Jambo hili linajumuisha wengi na mengi, kwa ufupi kunahitajika kuweko mikakati kabambe na inapaswa kuwa juu kwenye orodha ya vipaumbele vya jamii husika,patahitaji kueleweka na kufahamika kile kinachotakiwa kuandalia na wahusika,ikiwemo kuwepo kwa mitaala yenye kubeba hili lengo la kuweza kufikia kutayarisha wanazuoni kwa kuwepo wanazuoni waliokwisha fikia daraja hiyo;kwani asiekuwa na kitu hawezi kutoa kitu.
Hivyo basi huwa hakuna budiisipokuwa kuwepo mashirikiano baina ya wahusika. Hapa kunapendekezwa baadhi ya mikakati huenda ikawa muhimu na kupelekea kuweza kusaidia katika kufikia kutayarisha wanazuoni wakati wowote ule watakapopatikana na kubainika wale wenye kutarajiwa kuwa wanazuoni wa baadae.
Kumjenga kuimani, hili kwa mtazamo wa wengi linaonekana kuwa gumu sana,kwa kuwa linafungamana na moyo, hata hivyo hili ni jambo la msingi kwa kumtayarisha na kumuandaa mwanazuoni Ar Rabbaniy, jambo litaloweza kuleta matunda yatakiwayo kwa jamii ikiwa patajengwa na kupandikizwa mbegu madhubuti na thabiti ya imani.
Katika yenye kusaidia ni kule kuweza kugundu au mahiri wa walengwa na kuweza kuwachagua wenye muelekeo utakiwao.
Kushajiisha kusoma tarehe za wema waliotangulia zenye kufunua macho na nyoyo kwa lengo la kumzidishia imani na kuwa na nguvu.
Uwazi wa jambo, anapotakiwa kutayarishwa mtu kwa kazi kama hii yenye kufungamana na majukumu yaliyotangulia na mengineo, ni vyema kwa mtayarishwa aelezwa kwa uwazi kabisa yale atayokuja kukutana nayo katika hayo maandalizi na matayarisho. Kwani kutokana na maandalizi hayo atatarajiwa kuwa tayari kubadili majukumu kwa majukumu mazito zaidi, au kuengeza majukumu yake kwa kuja kubeba majukumu tofauti kabisa na yale aliyonayo. Hili ni muhimu sana kwa wanazuoni watarajiwa, kwani kuna siku moja watakuwa ndio wenye kushika hatamu za kutengeneza, kuisomesha jamii na kutatua matatizo yao kwa kutoa fatuwa na hukumu kulingana na mafundisho ya Dini.
Changamoto za hali halisi, kwa kuwa majukumu atayokuja kukabiliana nayomtayarishwa ni mazito, na ni yenye athari kwa kila upande, ni vyema kwa mwanachuoni mtarajiwa kuwekwa katika hali halisi ya majukumu hali itayoshinikiza na kumuweka uso kwa uso na utatuzi wa changamoto anazotarajiwa kukabiliana nazo hapo ataposhika wadhifa wake. Hivyo basi mijadala pia huhitajika katika kuwatayarisha wanazuoni wategemewa.
Kwa kuwapa changamoto wanazuoni watarajiwa kutasaidia kuongeza ustadi namaarifa yao ya kuweza kuelewa ule uwezo wao, na namna gani anaweza kujitumakatika kutafuta au kutafiti yale yenye kufungamana na tatizo husika, na piakutampa ujasiri wa kutoa hukumu kwa vile alivyoweza kulifananisha nakulifahamu.
Kuweka usaidizi, hili ni muhimu pia kwani wanazuoni watarajiwa, kwa kuwa watakuwa wanatoa hukumu na fatuwa ni vyema pakaweko na usaidizi utaofuatiliana kuthibitisha kile kinachotakiwa na kukirudisha kisichokuwa sahihi, kwani si kila hukumu watayoitoa itakuwa imesibu.
Ushauri, msaada na mafunzo ya ziada, mwanazuoni mtarajiwa atapenda kuona kuwa miongoni mwa mikakati ya kumtayarisha ni kuwa kuna wanazuoni wakumuendea kwa ushari, msaada na muongozo wa kitaalamu kwa kiwango cha hali ya juu utaoweza kumuelekeza kule anakotakiwa kufika, pia patahitaji kumuendeleza na kumsawazisha na pia kumpata utulivu, pongezi na ushajiishaji na hata ijaza.
Usimamizi angalifu na ufuatiliaji kamili, jambo la usimamizi angalifu na ufuatiliaji kamili ni muhimu katika kuandaa wanazuoni watarajiwa, kwani katikausimamizi angalifu kutapelekea kuweza kugundua yale yasiyoweza kugunduliwana usimamizi wa kawaida, yakiwemo matatizo yaliyofichikana na kutengenezapenye kutakiwa kutengenezwa.
Pia katika yenye kufungamana na haya ni kule kwa mtayarishwa kupewa nafasi ya kufanya mazoezi au majaribio ya jukumu lake jipya, kama vile kupatiwa fursa na mwanazuoni Ar Rabbaniy ya kudurusisha durusu au kujadili masuala yenye kupelekea kumjenga katika majukumu yake huku akifuatiliwa ufuatiliaji kamili, na kuangaliwa kwa uangalifu wa hali ya juu nahuyo mwanazuoni au kundi lenye kujumuisha wanazuoni Ar Rabbaniyyiyna.
Book an Online Session
I'm a paragraph. Click here to add your own text and edit me. I’m a great place for you to tell a story and let your users know a little more about you.