top of page

Acerca de

Kuhusu Sisi

Darsa Mihadhara Online ni mkusanyiko wa ndugu zetu wa kiislamu waliojikusanya kwa ajili ya kuinufaisha jamii ya kiislamu duniani kwa mafundisho ya dini kwa njia za mtandao.

Darsa Mihadhara Online imejifunga kikamilifu na Qur'aan na Sunnah kwa ufahamu wa Masahaba, Maimamu wa karne tatu bora za mwanzo na wale wenye kuwafuata kwa wema katika kutekeleza harakati zake.

 

Darsa Mihadhara Online imejikita kuelimisha jamii kupitia njia za mtandao kwa kuhakikisha kunapatikana Wahadhiri na Wadarisishaji wenye kutegemewa kutoka pembe zote za dunia.

 

 

Tovuti ya Darsa Mihadhara Online itapokea Mada, Mafundisho na Makala ambazo zitapitiwa na kuthibitishwa kisha kuwekwa kwenye tovuti ili ziwanufaishe waislamu watakaotembelea tovuti hii.

bottom of page